WADAU SHINYANGA WAKUBALIANA MAZAO JAMII YA MIKUNDE KUUZWA KWA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI
WADAU wa Mazao ya jamii ya Mikunde mkoani Shinyanga, wamekubaliana kwa pamoja mazao ya Choroko na Dengu kwamba katika msimu wa mwaka yauzwe kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ili kumuinua Mkulima kiuchumi.
Makubaliano hayo yameafikiwa leo Februari 15,2024 kwenye kikao cha wadau wa Mfumo wa Stakabadhi ghalani, kilicho husisha baadhi ya Wakulima wa Mazao hayo ya Mikunde,Wafanyabiashara,Viongozi mbalimbali wa Vyama vya Ushirika na Mabenki.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme,akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho, amesema mfumo wa Stakabadhi ghalani utachangia kuongeza uzalishaji wa mazao, ambapo Mkulima atapata fursa ya kuuza mazao yake kwa bei yenye faida na kuinuka kiuchumi, pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao kwa tija na ubora zaidi.
“Mfumo huu wa Stakabadhi Ghalani mazao yatakuwa yakiuzwa kwa njia ya Mnada na kuwa na ushindani zaidi kwa wafanyabiashara hali ambayo italeta uvumbuzi wa bei zenye tija kwa Wakulima, mfano zao la Korosho katika Mikoa ya Lindi na Mtwara bei imeimarika msimu hadi msimu na hii ni kutokana na matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani,”amesema Mndeme.
“Matumizi ya Mfumo huu kwenye Mkoa wetu kwa Mazao ya Choroko na Dengu ni dhahiri kuwa utaleta Manufaa Makubwa kwa Wakulima na Wafanyabiashara, niombe na Zao la Mpunga pia kuingizwa kwenye Mfumo wa Stakabadhi Ghalani ili Wakulima wa Zao hili waweze kunufaika zaidi ikiwa Mkoa wetu ni Miongoni mwa mikoa Mitatu inayozalisha zao hili kwa wingi,”ameongeza Mndeme.
Amesema Mfumo huo pia utawezesha Matumizi Sahihi ya Vipimo vya Mizani ambapo itamsaidia Mkulima asinyonywe pindi anapopeleka mazao yake kwenye Soko,pamoja na kuamsha Vyama Vya Msingi Sinzia na kukakikisha vinafanya kazi na hatimaye kuongezeka kwa uzalishaji wa Mazao yanayouzwa kupitia Mfumo wa Stakabadhi Ghalani.
Ameendelea kusema kwamba utekelezaji wa Mfumo huo utasaidia pia Serikali kupata Mapato, pamoja na Wakulima kupata Taarifa na Takwimu mbalimbali za Mazao kwa wakati na usahihi, pamoja na kuchochea huduma za kifedha vijijini ambapo Wakulima Malipo na Manunuzi yatapitia kwenye Taasisi za kifedha.
Naibu Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika na Udhibiti kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Collins Nyakunga, amesema Mfumo huo utaleta uwazi sababu utakusanya Mazao ya kuyapeleka kwenye Masoko,na kubainisha kwamba kwa nchi nzima kuna Jumala ya Vyama Vya Ushirika 7,391 na AMCOS 4,475 na Jumla ya Wanachama Milioni 12.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Asangye Bangu, amesema Mfumo huo utaleta bei ya ushindani kupitia Mnada na Wakulimwa watalipwa pesa zao ndani ya siku tatu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amesema Mfumo huo ni mzuri sababu umelenga kumuinua Mkulima kiuchumi, na kutoa wito kwa wasimamizi wa Mfumo huo kwamba wakawe Wazalendo na kumsaidia Mkulima.
Aidha,Mkuu wa Mkoa wakati akihitimisha Kikao hicho mara baada ya kumalizaka kwa majadiliano,aliuliza Wajumbe wote kama wamekubaliana Mazao hayo ya Mikunde Choroko na dengu yauzwe kwa Mfumo wa Stakabadhi Ghalani, ambapo walikubaliana, na Mfumo huo uanze msimu wa mwaka huu.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye Kikao hicho.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza kwenye Kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Asangye Bangu akizungumza kwenye Kikao hicho.
Naibu Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika na Udhibiti kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Collins Nyakunga akizungumza kwenye Kikao hicho.
Wadau wakiendelea na Kikao cha Mfumo wa Stakabadhi Ghalani kwa Mazao ya Mikunde.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Wadau wakiendelea na Kikao.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464