MADIWANI SHINYANGA WALIA NA MFUMO WA TAUSI UKUSANYAJI MAPATO YA HALMASHAURI

MADIWANI SHINYANGA WALIA NA MFUMO WA TAUSI UKUSANYAJI MAPATO HALMASHAURI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, wamelalamikia Mfumo wa Tausi wa ukusanyaji mapato, kwamba Mfumo huo umekuwa tatizo la ukusanyaji mapato ya halmashauri.
Wamebainisha hayo leo Februari 16, 2024 kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani cha Robo ya Pili mwaka wa fedha 2023/2024 cha kupitia taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo,pamoja na taarifa kutoka Kamati mbalimbali.

Wakijadili Taarifa ya Kamati ya Fedha na Utawala,baadhi ya Madiwani hao akiwamo Juma Nkwabi wa Mwawaza, wamelalamikia Mfumo wa Tausi wa ukusanyaji mapato kwamba umekuwa tatizo la kukwamisha kasi ya ukusanyaji mapato ya halmashauri sababu ya Mfumo kugoma kusoma, na hivyo wafanyabiashara kubaki na fedha zao mfukoni.
“Mfumo huu wa Tausi wa ukusanyaji Mapato ni tatizo, Mapato ya Halmashauri yanashuka toka Julai hadi leo mfumo unatatizo na hatujui ni lini utakaa vizuri ili tukusanye Mapato, wafanyabiashara wanashindwa kulipa Mapato yetu wanabaki na pesa zao mfukoni sababu ili walipe mapato lazima apewe namba ya malipo (Control namba) lakini mfumo hausomi,”amesema Nkwabi.

“Mfumo wa Tausi wa ukusanyaji Mapato ni tatizo, tunaomba Ofisi ya RAS Mkoa itusaidie kama kuna uwezekano wa kupata Kibali, ili tukusanye Mapato kwa wafanyabiashara na kuwapatia Risiti wakati tukisubili Mfumo wa Tausi ukae Vizuri,” ameongeza.
Naye Diwani wa Kizumbi Rubeni Kitinya, amekazia suala hilo la Mfumo wa Tausi la kukusanya Mapato, kwamba ni tatizo kubwa sababu unakwamisha halmashauri kupata mapato.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, naye amesisitiza kwamba Mfumo huo wa Tausi wa ukusanyaji Mapato unachangamoto kubwa katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Ibrahim Makana, amesema kwamba Mfumo huo wa Tausi wa ukusanyaji mapato ni mzuri, isipokuwa Changamoto inajitokeza kwa Mtumiaji Mmoja Mmoja, na kubainisha kwamba hakuna Mapato ambayo yatakusanywa nje ya Mfumo huo.

Aidha, amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze, kwamba waendelee kutoa elimu juu ya Matumizi ya Mfumo huo wa Tausi wa ulipaji Mapato ili ulete tija, pamoja na kusimamia vizuri kitengo cha ukusanyaji mapato na kuwabidilisha Watumishi wa kitengo hicho mara kwa mara.

TAZAMA PICHA ZA KIKAO CHA BARAZA HAPA CHINI👇👇
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye Kikao hicho cha Baraza la Madiwani.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Ibrahim Makana akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani.
Kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga kikiendelea.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464