KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA (PIC) YATEMBELEA YADI YA MTAMBO WA USAFIRISHAJI WA MAFUTA GHAFI

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA (PIC) YATEMBELEA YADI YA MTAMBO WA KUANDAA MABOMBA

Na Shaban Njia, NZEGA.

KAMATI ya kudumu ya Bunge Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imetembelea yadi ya mtambo wa kuandaa mabomba yatakayotumika katika usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, unaojengwa katika kijiji cha Sojo kata ya Igusule Wilaya ya Nzenga mkoani Tabora.

Ziara hiyo imefanyika leo Februari 19,2024 ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Deus Sangu amabayo pia ilitembelea kuona ujenzi wa kiwanda unavyoendelea ikiwa nipamoja na kutoa ushauri namna ya kuvituhudumia vijijini vinavyozunguka mradi huo kwa kutoa ajira kwa vijana zisizohitaji ujuzi wowote.

Sangu ambaye pia ni Mbunge wa Gwela akizungumza kwenye ziara hiyo amesema pamoja na mambo mengine ambayo watakwenda kuyajadili kwenye kamati yao baada ya kumaliza ziara yako mikoa mengine, ameipongeza Wizara ya Nishati kwa kuhakikisha mradi hausuisui kwa kutoa fedha kwa wakati kwa wakandarasi wake.

Amesema, wanaridhiwa na kasi ya ujenzi wa yadi ya mtambo wa kuandaa mabomba yatakayotumika kusafirishia mafuta ghafi na kuwataka kuyatunza mazingira na viumbe vilivyopo kwani awali mradi huo ulikuwa na kelele nyingi zilizotaka kukwamisha mradi lakini kutokana na usimamizi mzuri uliopo bado upo na utakamilika kwa wakati.

Pia Sangu ameitaka Wizara ya Nishati kusimamia juu ya ulipaji wa ushuru wa huduma na CSR kwani kumekuwa na malalamiko ya uwepo wa kampuni mmoja inayolipa fedha hizo huku nyingi zikiwa hazilipi na baadhi zimeshamaliza mikataba yao na kuondoka na kuwasisitiza kuyafuatilia ili walipe fedha walizotakiwa kuzilipa.

“Tunaomba kupata orodha ya makapuni yote yanayofanyakazi na mradi huu ili tufahamu yapi yanayolipata ushuru wa huduma kwenye halmashauri zetu na managapi hayalipi na kwanini na tunatoa muda wa siku saba tuwe tumepata orodha yake, tunataka ziara yetu iwe neema kwa halmashauri zote ambazo mradi huu unapita”Ameongeza Sangu.

Mratibu wa mradi wa ECOP Taifa Kisamarwa Joseph amesema, mradi huo ulianza mwaka 2021 na unatarajia kukamilika disemaba 2025 asilimia kubwa ya wafanyakazi ni wazawa kulinganisha na wageni ambao ni asilimia sita pekee na wengi wanatoka kijiji cha Sojo, Nzega, Tabora, Isagehe, Kagongwa na mkoa wa Shinyanga.

Amesema,shughuli za usafirishaji mabomba zinajumuisha usafirishaji kwa njia ya meli kutoka kwa mtengenezaji aliyepo nje ya nchi hadi bandari ya Dar es Salaam ambako yatashushwa na kusafirishwa kwa magari maalum hadi kwenye kituo cha kupokelea mabomba kilichopo Dar Es Salaam na kisha kuyasafirisha mabomba hayo kwa njia ya barabara hadi Kituo cha Kagongwa.

Aidha amesema, kati ya mambo muhimu yaliyofikiwa na mradini pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa nyumba mbadala339 kwa ajili ya kaya 344 zilizopoteza makazi, ambapo nyumba 12 zilijengwa hapa katika Kijiji cha Sojo. Nyumba hizo zilijengwa na wakandarasi wazawa kwa kutumia vifaa na vibarua wa kutoka katika jamii.

Pia Joseph amesema, mradi umefanikiwa kutia saini na kulipa fidia kwa asilimia 99 ya Watu 9,904 walioguswa na Mradi (PAPs), na kuonyesha dhamira ya dhati ya kushughulikia kwa wakati kero na mahitaji ya watu walioguswa na mradi.

Vilevile amedai kuwa, mradi unapanga kuboresha barabara mbalimbali zinazofika maeneo ya Mradi ikiwa ni pamoja na kilomita 7.4 za barabara ya Murram kutoka barabara ya Mombasa hadi Chongoleani na kilomita 18.6 kutoka Kagongwa hadi Mtambo wa Kupaka Rangi Mabomba wa Sojo. Aidha, upanuzi wa mtandao wa maji umefanyika katika mikoa mbalimbali kama vile RUWASA – Kagera, HTM WSSA- Handeni na Tanga UWASA.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Sojo Kata ya Igusule Wilaya ya Nzega mkoani Tabora Boniphace Mikongi ameomba Kamati kusimamia na kuhakikisha mradi unajenga bweni la wanafunzi katika sekondari sojo ili kuwanusuru wanafunzi wa kike na mimba ili kutimiza ndoto zao kwani kunavijana wengi wametapakaa mitaani hali inayowatia hofu ya kuwarubuni wanafunzi hao.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464