NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA DK. GRACE MAGEMBE,AMETOA MAAGIZO MAZITO KWA WATUMISHI WA AFYA SHINYANGA
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Grace Magembe,amefanya ziara mkoani Shinyanga,na kutoa Maagizo kwa Watumishi wa Afya kutoa huduma stahiki za matibabu kwa wagonjwa.
Amefanya ziara hiyo leo Februari 23,2024, kwa kuona utoaji wa huduma za Afya katika Kituo cha Afya Kambarage,Ujenzi wa OPD Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga, na huduma za matibabu hospitali ya Rufaa Mkoa pamoja na kuzungumza na Watumishi wa Afya.
Amesema Serikali imeboresha utoaji wa huduma za Matibabu kwa wananchi,kwa kujenga Zahanati,Vituo vya Afya, hospitali pamoja na kutoa vifaa tiba vya kisasa, na hivyo kuwataka Watumishi wa Afya kutoa huduma stahiki za matibabu kwa Wagonjwa.
Amesema katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Serikali itaongeza pia ujenzi wa Majengo 5 ili kuboresha huduma za Matibabu, ikiwamo ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto,Maabara, Stoo ya dawa, Mochwari na Jengo la kufua nguo za wagonjwa.
Tunataka Maboresho haya ya huduma za Afya, yaendane na utoaji wa huduma bora za matibabu kwa wananchi," amesema Dk. Magembe.
Katika hatua nyingine ametoa Maagizo kwa Watumishi wa Afya, kuzingatia Miiko,Sheria,kanuni na maadili ya taaluma zao pamoja na kutunza siri za wagonjwa.
Amesema kwa Mtumishi wa Afya ambaye anakwenda kinyume na Maadili ya Taaluma yake na kuitia doa Sekta hiyo, hawata sita kumchukulia hatua kwa kumuondoa kazi na hata kufutiwa Leseni yake.
Pia ameagiza ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga,kwamba ukamilike kwa wakati ili lianze kutumika kutoa huduma kwa wananchi, ambalo linatarajiwa kukamilika Marchi mwaka huu.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga DK.Yudas Ndungile, ameipongeza Serikali kwa kuboresha huduma za Afya mkoani humo,na kwamba baadhi ya huduma ambazo Wananchi walikuwa wakienda kupata Bugando Jijijini Mwanza,sasa hivi zinapatikana mkoani humo.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako, amesema maelekezo yote ambayo yametolewa watayafanyia kazi, ili kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Grace Magembe akizungumza na Watumishi wa Afya wa Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Grace Magembe akiendelea kuzungumza na Watumishi wa Afya mkoani Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Grace Magembe akizungumza na wagonjwa katika Kituo cha Afya Kambarage.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Grace Magembe, akiangalia Kifaa Tiba cha Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Kambarage ambacho kitafanya uchunguzi wa Meno na kutoa Tiba na siyo kung'oa meno tena.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Grace Magembe akiangalia uandikishaji wa Wagonjwa kwa mfumo wa Mtandao katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Grace Magembe akiendelea kukagua ubora wa utoaji huduma katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Grace Magembe akikagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje OPD katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Grace Magembe akifuatilia huduma za mapokezi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Grace Magembe akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Grace Magembe akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Grace Magembe akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Grace Magembe akiangalia namna uzalishaji wa Hewa ya Oxgyen katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Grace Magembe akizungumza na wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Watumishi wa Afya wakiwa kwenye kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Grace Magembe wakisikiliza maelekezo ya Serikali juu ya utoaji wa huduma bora ya matibabu kwa wananchi.
Watumishi wa Afya wakiwa kwenye kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Grace Magembe wakisikiliza maelekezo ya Serikali juu ya utoaji wa huduma bora ya matibabu kwa wananchi.
Watumishi wa Afya wakiwa kwenye kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Grace Magembe wakisikiliza maelekezo ya Serikali juu ya utoaji wa huduma bora ya matibabu kwa wananchi.
Watumishi wa Afya wakiwa kwenye kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Grace Magembe wakisikiliza maelekezo ya Serikali juu ya utoaji wa huduma bora ya matibabu kwa wananchi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464