Header Ads Widget

RC MNDEME KUANZA ZIARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI NA KUZITATUA

RC MNDEME KUANZA ZIARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI NA KUZITATUA 

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, anatarajia kuanza ziara ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Akizungumza leo Februari 27,2024 na Waandishi wa Habari wakati akitoa Ratiba ya ziara hiyo, amesema ziara itaanza kesho Februari 28 Manispaa ya Shinyanga,Mkutano utakaofanyika kuanzia Majira ya Saa 5 asubuhi katika maeneo ya Soko Kuu.

Amesema Februari 29 atakuwa Manispaa ya Kahama kwakusikiliza kero za wananchi na kuzitatua, Mkutano utakaofanyika Kata ya Majengo.

Amesema Marchi 1 Majira ya saa 4 asubuhi atafanya Mkutano Kata ya Kakola, na Majira ya Saa 8 atakuwa Kata ya Segese zote za Halmashauri ya Msalala, kwa kusikilzia kero za wananchi na kuzitatua.

“Nitumie fursa hii kuwakaribisha wananchi wenye kero mbalimbali, maoni na ushauri wafike kwenye Mikutano hii ili Changamoto zao zitatuliwe, wananchi wote tunawakaribisha waje kwa wingi,”amesema Mndeme.

Post a Comment

0 Comments