DC MKUDE AWABANA MAAFISA ELIMU KISHAPU KUELEZA SABABU HALMASHAURI KUTOFANYA VIZURI KITAALUMA


MKUU wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude,amewataka Wakuu wa Idara za Elimu Msingi na Sekondari wilayani humo,kutoa taarifa za utekelezaji wa Majukumu yao katika Sekta ya Elimu, na kueleza Changamoto zinazosababisha Halmashauri ya Kishapu kutofanya vizuri Kitaaluma.

Amebainisha hayo leo Februari 22,2024 wakati akitoa Hotuba ya kufunga kikao cha wadau wa Elimu wilayani humo katika Ukumbi wa Hotel ya Stage 2.
Mkude akizungumza kwenye Kikao hicho amewataka Wakuu wa Idara za Elimu za Msingi na Sekondari wilayani humo, kutoa taarifa za utekelezaji wa majukumu yao, pamoja na kutafutia ufumbuzi Changamoto ambazo zinasababisha halmashauri ya Kishapu kushuka Kitaaluma ili kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kwa shule za Msingi na Sekondari.
Aidha, amewapongeza pia Wamiliki wa shule Binafsi wilayani humu ambao wameamua kuwekeza kwenye Sekta ya Elimu huku akiahidi kwamba Serikali itaendelea kuwaunga Mkono.

Kwa upande wao Wakuu wa Idara za Elimu Msingi na Sekondari kwa nyakati tofauti tofauti walieleza changamoto mbalimbali katika ufundishaji na ujifunzaji ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa Shule za Msingi na Shule za kutwa kwa Shule za Sekondari kutokupata chakula cha mchana hivyo wanafunzi kukosa usikivu katika kujifunza.
Wamesema hali hiyo imekuwa ikisababisha wanafunzi kuwa na Msingi mbaya wa masomo tangu wakiwa vidato vya chini hali inayopelekea kuwa na ufaulu duni katika masomo yao.

Baada ya kuwasilishwa kwa changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu katika Mkutano wa wadau wa Elimu, Mwenyekiti aliruhusu mjadala wa wazi kwa wadau wa Elimu katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo ili kuweza kuinua ufaulu wa wanafunzi.
Wajumbe wa Mkutano huo walichangia hoja mbalimbali kama suluhisho na mwarobaini wa kuinua kiwango cha Elimu sanjari na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika shule za Msingi na Sekondari kama madarasa,maabara,nyumba za walimu,upatikanaji wa walimu wa sayansi,madawati na motisha kwa walimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kishapu Ndugu Emmanuel Johnson aliwapongeza wadau wa Elimu kwa kuzichambua changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu na kuwataka wadau wa Elimu kufanya kazi bega kwa bega na Halmashauri na wadau mbalimbali wa Elimu katika kutatua kero zinazoweza kuipandisha taaluma na hatimaye kutoka hatua tuliyonayo kwenda hatua nyingine.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Ndg. Shija Ntelezu alitoa maoni yake kwa kuwataka wazazi kama wadau wakubwa wa kuinua ufaulu wa mtoto kutimiza wajibu wao na siyo kuwaachia walimu pekee katika suala la kumlea mtoto.

Wazazi tutimize wajibu wetu katika kuinua kiwango cha Elimu kwa watoto wetu pasipo kuwaachia walimu pekee,mwalimu ana nafasi yake katika kumlea mtoto na mzazi pia ana wajibu wake, tukitekeleza wajibu wetu kiwango cha Elimu kitapanda,"Ntelezu amesema.
Aidha Mwenyekiti wa Mkutao huo Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude aligawa Tuzo kwa Shule zilizofanya Vizuri Katika Mitihani kwa mwaka 2023.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halamshauri Wiliamu Jijimya akizungumza kwenye Kikao hicho.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu Emmanuel Johnson akizungumza kwenye Kikao hicho.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu akizungumza kwenye Kikao hicho.
Viongozi wakiwa Meza Kuu.
Viongozi wakiwa Meza Kuu.
Mijadala ikiendelea kwenye Kikao hicho.
Mijadala ikiendelea kwenye Kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Vyeti vya pongezi zikitolewa.
Vyeti vya pongezi vikiendelea kutolewa.
Vyeti vya pongezi vikiendelea kutolewa.
Vyeti vya pongezi vikiendelea kutolewa.
Picha za pamoja zikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464