KAMATI YA USALAMA BARABARANI MKOA WA SHINYANGA YAKABIDHI GARI LA DORIA
Na Mapuli Kitina Misalaba
Kamati ya usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga imekabidhi Gari aina ya TOYOTA KULDER STATION WAGON yenye namba T530 EFP, lenye thamani ya Shilingi Milioni 29 kwa ajili ya kurahisisha doria mbalimbali za Barabarani.
Gari hilo limekabidhiwa Jana kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi na mwenyekiti wa kamati ya usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga Bwana Wilson Majiji kwa niaba ya kamati hiyo.
Akikabidhi gari hilo Mwenyekiti wa Kamati ya usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Bwana Wilson Majiji amelitaka jeshi hilo la Polisi Mkoa wa Shinyanga kulitumia Gari hilo vizuri kwa ajili ya kurahishaji doria mbalimbali za Barabarani katika kudhibiti ajali zisizokuwa za lazima na kuhakikisha Mkoa unakuwa salama.
Kwa upande wake kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Janeth Magomi ameishukuru kamati hiyo ya usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga na kuahidi kulitumia gari hilo kwa shughuli iliyokusudiwa ili kuhakikisha ajali za Barabarani zinapungua na kuufanya Mkoa wa Shinyanga kuwa salama.
Muonekano wa Gari ambalo limenunuliwa na kamati ya usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Polisi kitengo cha usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga SSP Wenceslaus Deus akisoma taarifa ya ununuzi wa Gari la kamati ya usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa kamati ya usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga Bwana Wilson Majiji akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi Gari.
Mjumbe wa kati ya usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Joel Mwambungu akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi Gari.