RC MNDEME ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI MANISPAA YA SHINYANGA NA KUZITAFUTIA UFUMBUZI
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme,amesikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Shinyanga na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkutano huo wa kusikiliza kero za wananchi umefanyika leo Februari 28,2024 katika Soko kuu la Manispaa ya Shinyanga.
Mndeme akizungumza wakati wa kutatua kero hizo za wananchi, amewataka Watumishi wa Serikali wafanye kazi kwa weledi katika kuwahudumia wananchi.
Aidha, akijibu kero ya kutokamilika kwa Soko Kuu la Manispaa ya Shinyanga, ametoa maelekezo kwamba hadi kufikia Mei 30 mwaka huu Soko hilo liwe limeshakamilika kujengwa lote na kuanza kutumika, na siyo Mwezi Julai kama alivyosema Mkurugenzi.
Amewataka pia Watumishi wa Idara ya Ardhi kufanya kazi zao kwa weledi na umakini ili kuepusha migogoro ya ardhi, ikiwamo kutogeuza matumizi ya ardhi kinyume na utaratibu.
“Kero zote ambazo mmeziwasilisha hapa zitashughulikiwa kwa utaratibu na kila mtu atapata haki yake,”amesema Mndeme.
Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi,akijibu kero ya Mikopo umiza, amewataka wananchi wajiepushe na Taasisi ambazo zinakopesha fedha zisizo na vibali wala kutambulika na BOT, na kwamba watakapopata taarifa za Taasisi isiyo sajiliwa wampatie taarifa.
Aidha, kwenye Mkutano huo wa Mkuu wa Mkoa, zimesikilizwa kero mbalimbali ikiwamo Migogoro ya Ardhi, Mirathi, Kazi, Mikopo Umiza, Mafao, utelekezaji watoto, ujenzi wa Masoko kutokamilika, kubambikiziwa kesi, kupanda bei ya Sukari, umeme na ubovu wa miundombinu ya barabara hasa ya kutoka Ndala kwenda Hospitali ya Rufaa Mwawaza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, kesho ataendelea na ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi katika Manispaa ya Kahama Mkutano utakaofanyika Kata ya Majengo.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye Mkutano wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea kuzungumza kwenye Mkutano wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea kuzungumza kwenye Mkutano wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akijibu baadhi ya kero za wananchi kwenye Mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akijibu baadhi ya kero za wananchi kwenye Mkutano huo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze akijibu kero kwenye Mkutano huo.
Mwamba Masanja kutoka Takukuru akijibu baadhi ya kero kwenye Mkutano huo.
Viongozi wakiwa meza kuu kwenye Mkutano wa kusikiliza kero za wananchi wa Manispaa ya Shinyanga na kuzitafutia ufumbuzi.
Watumishi mbalimbali wa Serikali wakiwa kwenye Mkutano wa kusikiliza kero za wananchi.
Watumishi mbalimbali wa Serikali wakiwa kwenye Mkutano wa kusikiliza kero za wananchi.
Watumishi mbalimbali wa Serikali wakiwa kwenye Mkutano wa kusikiliza kero za wananchi.
Wananchi wakitoa kero zao kwenye Mkutano huo.
Wananchi wakiendelea kupaza kero zao kwenye Mkutano huo.
Wananchi wakiendelea kutoa kero zao.
Wananchi wakiendelea kutoa kero zao.
Wananchi wakiendelea kutoa kero zao.
Wananchi wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa kutoa kero zao kwa Mkuu wa Mkoa na kutafutiwa ufumbuzi.
Wananchi wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa kutoa kero zao
Mkutano ukiendelea.
Wananchi wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa kutoa kero zao.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464