BENKI YA TCB IMEKABIDHI MATUNDU 12 YA VYOO, CHUMBA MAALUMU CHA KUJISTIRI HEDHI SHULE YA SEKONDARI BUSIYA KISHAPU
BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) Tawi la Shinyanga imekabidhi Matundu 12 ya vyoo na Chumba Maalumu cha kujistiri hedhi kwa wanafunzi wa kike, katika Shule ya Sekondari Busiya Kata ya Itilima wilayani Kishapu.
Makabidhiano ya Matundu hayo 12 ya vyoo na Chumba Maalumu cha kujistiri hedhi yamefanyika leo Februari 29,2024 shuleni hapo na kuhudhuliwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Kishapu David Mashauri akimwakilisha Mkurugenzi.
Meneja wa Benki ya TCB Tawi la Shinyanga Julius Mataso, akizungumza kabla ya kukabidhi Matundu hayo 12 ya vyoo na Chumba Maalumu cha kujistiri hedhi, amesema kwamba mwaka 2021alialikwa kuwa mgeni Rasmi katika Mahafari ya kidato cha Nne na kukumbana na Changamoto ya hali mbaya ya huduma ya Choo shuleni hapo.
Amesema kutokana na Benki hiyo kuwa wadau wakubwa wa Elimu na wamekuwa wakiunga Mkono Serikali, wakaguswa na kuamua kujenga Matundu hayo ya vyoo 12 na Chumba Maalumu cha kujistiri hedhi, ili wanafunzi wasome katika Mazingira Rafiki.
“Benki ya TCB hua tuna Miradi ya Maendeleo kwa Jamii kurudisha sehemu ya faida ambayo tunaipata CSR hasa katika maeneo matatu ya Elimu, Afya na Maji, ndipo tukaamua kujenga Matundu haya 12 ya vyoo na chumba cha kujistiri hedhi ili kunusuru afya za wanafunzi.”amesema Mataso.
Aidha, ametaja gharama ya ujenzi wa Matundu hayo 12 ya vyoo na Chumba Maalumu kwa wanafunzi wa kike kujistiri hedhi kuwa ni Sh.milioni 33.7, na ujenzi wake ulianza Oktoba mwaka jana na umekamilika Februari mwaka huu.
Mkuu wa shule hiyo ya Sekondari Busiya Badi Mfinanga, ameishukuru Benki hiyo kujenga Matundu hayo ya vyoo 12 na Chumba Maalum cha wasichana, kwamba Shule hiyo inajumla ya wanafunzi 351 wavulana 176 na wasichana 175, na walikuwa wakitumia Matundu Sita ya Choo, Matatu Wasichana, na Matatu Wavulana huku Choo kikiwa katika hali mbaya.
Naye Mgeni Rasmi Afisa Elimu Halmashauri ya wilaya ya Kishapu David Mashauri akimwakilisha Mkurugenzi, amesema Matundu hayo ya vyoo 12 na Chumba maalumu cha kujistiri hedhi, itakuwa ni chachu kubwa ya kuinua Taaluma ya wanafunzi shuleni hapo sababu watasoma katika Mazingira Rafiki.
“Tunawashukuru wadau Benki ya TCB kwa kuiunga Mkono Serikali na kutatua Changamoto ya uhaba wa Matundu ya vyoo katika shule hii ya Sekondari Busiya, na sisi tutaleta huduma ya maji shuleni hapa, na vyoo hivi vitunzeni na viwe visafi muda wote na vidumu kwa muda mrefu,”amesema Mashauri.
Nao baadhi ya wanafunzi katika shule hiyo akiwamo Mary Richard, wameshukuru ujenzi wa Matundu hayo ya vyoo 12 na Chumba Maalumu cha kujistiri hedhi, kwamba itawasaidia kufanya vizuri kwenye masomo yao na kuachana na utoro wa rejareja hasa wanapokuwa katika siku zao.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Meneja wa Benki ya TCB Tawi la Shinyanga Julius Mataso akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Matundu 12 ya vyoo na Chumba Maalumu cha kujistiri hedhi wanafunzi wa kike.
Mgeni Rasmi David Mashauri akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Matundu 12 ya vyoo na Chumba cha kujistiri hedhi kutoka Benki ya TCB.
Diwani wa Itilima wilayani Kishapu Lameck Dotto akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Busiya Badi Mfinanga akizungumza kwenye hafla hiyo.
Viongozi wakiwa meza kuu kwenye hafla hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Busiya wilayani Kishapu wakiwa kweye hafla ya Shule hiyo kukabidhiwa Matundu 12 ya vyoo na Chumba Maalumu cha kujistiri hedhi kutoka Benki ya TCB.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Busiya wilayani Kishapu wakiwa kweye hafla ya Shule hiyo kukabidhiwa Matundu 12 ya vyoo na Chumba Maalumu cha kujistiri hedhi kutoka Benki ya TCB.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Busiya wilayani Kishapu wakiwa kweye hafla ya Shule hiyo kukabidhiwa Matundu 12 ya vyoo na Chumba Maalumu cha kujistiri hedhi kutoka Benki ya TCB.
Hafla ikiendelea.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Busiya wilayani Kishapu wakiwa kweye hafla ya Shule hiyo kukabidhiwa Matundu 12 ya vyoo na Chumba Maalumu cha kujistiri hedhi kutoka Benki ya TCB.
Mgeni Rasmi Afisa Elimu Sekondari wilayani Kishapu David Mashauri (kulia) akifungua jiwe la msingi katika hafla ya kukabidhiwa Matundu 12 ya vyoo na Chumba Maalumu cha kujistiri hedhi kutoka Benki ya TCB (kushoto) ni Meneja wa Benki hiyo Julius Mataso.
Mgeni Rasmi Afisa Elimu Halmashauri ya Kishapu David Mashauri (kulia) akishikana Mkono na Meneja wa Benki ya TCB Tawi la Shinyanga Julius Mataso ikiwa ni ishara ya kukabidhiana Matundu 12 ya vyoo katika shule ya Sekondari Busiya.
Muonekano wa Matundu Sita ya Choo cha Wasichana na chumba Maalumu cha kujistiri hedhi.
Muonekano wa Matundu Sita ya Choo cha Wavulana.
Muonekano wa Chumba Maalumu cha wanafunzi wenye uhitaji.
Muonekano wa Choo cha zamani shuleni hapo.
Picha za pamoja zikipigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.