Shinyanga
WADAU wa zao la Choroko mkoani Shinyanga wakubaliana kuuza zao hilo kwa mfumo wa Stakabadhi za ghala ili kuwawezesha wakulima kupata faida kubwa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Chrisrtina Mndeme amewaagiza maofisa kilimo na wale wa ushirika kusimamia mfumo huo ili kuhakikisha unafanikiwa.
"Niwaombe maofisa ushirika wote pamoja na maofisa kilimo wote hakikisheni mnasimamia mfumo huu ili ufanikiwe, na ninaagiza wale wote walioko kwenye vizuizi, msiruhusu choroko au dengu kusafirishwa iwapo hazikupitia kwenye mfumo,"
"Lengo la Serikali ni kuhakikisha inamkomboa mkulima, hasa hawa wa mazao ya jamii ya mikunde, sasa ikibainika mnunuzi hakufuata mfumo wa Stakabadhi za ghala naagiza akamatwe, ameeleza Mndeme.