Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionyesha vifaa alivyokamata kwa waganga
Suzy Butondo,Shinyanga press blog
Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga limefanikiwa kukamata sukari mifuko nane ya Kagera sugar, na watuhumiwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukamata nyaya za umeme rola mbili za mradi wa Rea, pamoja na vifaa mbalimbali.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga SACP Janeth Magomi akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo februari 28,2024 ofisini kwake, amesema mifuko ya sukari hiyo imekamatwa juzi Wilayani Kahama wakati jeshi la polisi wakati likiendelea kufanya doria na misako mbalimbali ili kuzuia uhalifu.
Magomi amesema katika doria na misako iliyofanyika kati ya januari 21,2024 hadi Februari 27, 2024 amesema wamefanikiwa kukamata sukari mifuko nane ya Kagera sugar nyaya za umeme rola mbili za mradi wa Rea, Tv 06 piki piki tatu, Sola panel moja, nondo sita na mashine moja ya kusukuma maji.
Vitu vingine ni viti 12, Deck moja,meza mbili, frem tano za meza ngozi moja ya nyoka aina ya chachu redio mbili,bhangi gram 2190 kete 23 namisokoto 121 ambazo zimepelekwa kwamkemia mkuu wa serikali kwa ajili ya uchaguzi,pombe ya moshi lita 11 pamojana mitambo miwili ya kutengeneza pombe ya moshi.
"Pia tumefanikiwa vifaa mbalimbali vya kupigia ramli chonganishi na watuhumiwa 40 ambao walikamatwa katika vituo mbalimbali mkoani hapa,"amesema Magomi.
Katika upande wa mahakamani jumla ya kesi 10 zimepata mafanikio ambapo kesi moja ya kulawiti mshitakiwa alihukumiwa kifungo cha maisha jela, kesi moja ya unyang'anyi wa kutumia nguvu washitakiwa wawili walihukumiwa kifungo cha maishajel, kesi moja ya kubaka mshitakiwa alihukumiwa miaka 30 jera, kesi moja ya ukatili dhidi ya mtoto, ambapo mshitakiwa alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.
Amesema kesi mbili za wizi washtakiwa wawili walihukumiwa kifungo cha miezi sita jela, kesi mbili za kufanya shughuli za uganga bila kibali washitakiwa wawili walihukumiwa kifungo cha miezi sita jela na kesi moja ya shambulio la kudhuru mwili, mshitakiwaalihukumiwakifungo cha miezi mitano jela.
Aidhakatika kuhakikisha ajali za barabarani zinadhibitiwa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kitengo cha usalama barabarani limefanikiwa kukamata jumla yamakosa 5,026 ambapo makosa ya magari ni 3,781 na makosa ya pikipiki pamoja na bajaji ni 1,245 ambapo watuhumiwa waliwajibishwa kwa kulipa faini za papo kwa papo.
"Katika matukio hayo jumla ya madereva watatu walifungiwa leseni zao za udereva kwa kipindi cha miezi mitatu kwa kusababisha ajali, kuebdesha mwendokasi namatumizi mabaya ya barabara, pia jeshi lapolisi linawashukuru wananchi kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika kudhibiti uhalifu kwa kutoa taarifa"amesema Magomi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464