KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MGODI WA ALMASI MWADUI

Kamati ya kudumu ya Bunge Nishati na Madini yatembelea Mgodi wa Almasi Mwadui

Na Marco Maduhu, KISHAPU

KAMATI ya kudumu ya Bunge Nishati na Madini,yatembelea Mgodi wa Almasi Mwadui wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, ikiwamo kuona nyumba za fidia za Waathirika wa bwawa la Majitope, pamoja na Bwawa Jipya la Majitope ambalo linatumika katika uzalishaji wa Almasi.
Ziara hiyo imefanyika leo Februari 18,2024 ikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Shabani Ng'enda, ambayo pia ilitembelea kuona Shimo la uchimbaji wa madini ya Almasi.

Ng'enda akizungumza kwenye ziara hiyo, amesema pomoja na mambo mengine ambayo watakwenda tujadili kwenye Kamati,ameupongeza Mgodi huo wa Mwadui kwamba tangu kutokea tukio hilo la bwawa kupasuka,wamekuwa pamoja na wananchi na kuwapatia huduma mbalimbali ikiwamo kuwalipa fidia.
"Kamati tumetembelea kuona nyumba ambazo Wananchi wamelipwa fidia,na Sisi kama Kamati ya kudumu ya Bunge Nishati na Madini, tutakwenda kukaa kujadili,wananchi endeleeni kuwa watulivu, tunaupongeza pia Mgodi tangu tukio hili litokee mmekuwa pamoja na wananchi na kuwapatia huduma mbalimbali za kijamii na kuwalipa fidia,"
 amesema Ng'enda.

"Nyumba ambazo Wananchi wamelipwa fidia tumeona zina ubora kuliko zile ambazo walikuwa wakiishi awali, tunacho shauri ziboreshwe kwa kuongezewa Mlango wa Pili," ameongeza.
Aidha, aliishauri pia Serikali kufanya mapitio upya ya tathimini  eneo la Madhira na Mchakato wa wananchi kulipwa fidia ili kuondoa Manung'uniko yaliyopo, pamoja na Wizara ya Madini iwasilishe Kitabu cha fidia kwenye Kamati yao juu ya fidia ambayo wananchi wamelipwa.

Amesema pia Kamati hiyo wameitaka Wizara ya Madini isimamia juu ya ulipaji wa CSR kutokana na kiwango cha uzalishaji wa Mgodi, licha ya kwamba Mgodi huo ni walipaji wazuri wa CSR, pamoja na kuharakisha mchakato wa kuongeza asilimia ya umiliki wa Ubia wa Mgodi huo kutoka asilimia 25 hadi 37.

Naye Diwani wa Mwadui Luhumbo Francis Manyanda, akijibu swali aliloulizwa na Katamati hiyo juu ya wananchi kushirikishwa ulipwaji fidia, amesema kwamba jambo hilo lilikuwa na uwazi na wote wameshirikishwa hadi hatua ya mwisho.
Nao baadhi ya wananchi ambao ni wanufaika wa nyumba hizo za fidia akiwamo Suzana Ngussa, amesema wamefarijika kujengewa nyumba hizo imara, na kutoka kuishi kwenye nyumba za tope.

Naye Afisa Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Bernard Mihayo, amesema kwamba nyumba za fidia ambazo zilipaswa kujengwa ni 48 na 42 zimekamilika na wananchi wameanza kuishi, mbili ujenzi wake unaendelea,ambapo nyumba Nne wananchi wamegoma wakitaka walipwe fidia ya pesa.
Kaimu Meneja wa Mgodi wa Almasi Mwadui Mhandisi Shaghembe Mipawa, ambaye ni Mhandisi Mkuu wa Mgodi huo, amesema kwamba tukio hilo la kubomoka Bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui likitokea November 7 Mwaka 2022, na kuathiri wananchi 286 katika Kaya 50 wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze na wamelipwa fidia.

Amesema baada ya tukio hilo, walikuwa pamoja na wananchi kwa kuwapatia huduma zote za Kijamii ikiwamo Chakula, Maji, Makazi na Malazi pamoja na Watoto kuwapeleka Shule.
Aidha, amesema uzalishaji Rasmi wa Almasi kwenye Mgodi huo ulianza Julai 15 Mwaka Jana, mara baada ya kumalizika kujengwa kwa Bwawa Jipya la kihifadhia Majitope

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Shabani Ng'enda wa Kamati kudumu ya Bunge Nishati na Madini Shabani Ngenda akizungumza kwenye ziara hiyo.
Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shaghembe Mipawa akitoa maelezo kwenye ziara hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini.
Afisa Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo akitoa maelezo kwenye ziara hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini.
Mwananchi Suzana Ngussa akielezea namna walivyolipwa Fidia za Nyumba.
Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shaghembe Mipawa akielezea namna walivyojenga bwawa Jipya la kuhifadhia Majitope na kuanza uzalishaji wa Madini ya Almasi,mara baada ya bwawa la awali kupasuka.
Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shaghembe Mipawa akielezea namna walivyojenga bwawa Jipya la kuhifadhia Majitope na kuanza uzalishaji wa Madini ya Almasi, mara baada ya bwawa la awali kupasuka.
Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shaghembe Mipawa akielezea namna walivyojenga bwawa Jipya la kuhifadhia Majitope na kuanza uzalishaji wa Madini ya Almasi, mara baada ya bwawa la awali kupasuka.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini wakiwa kwenye bwawa la Majitope la zamani ambalo lilipasuka Kingo zaake.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini wakiwa kwenye Shimo la kuchimba Madini ya Almasi.
Muonekano wa Shimo la kuchimba Madini ya Almasi.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini wakiangalia nyumba walizolipwa fidia wananchi ambao waliathirika na Bwawa la Majitope.
Muonekano wa Baadhi ya nyumba ambazo wananchi wamelipwa fidia.
Muonekano wa baadhi ya nyumba ambazo wananchi wamelipwa fidia.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464