Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Masha Mshomba, ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma, tarehe 15 Februari, 2024.
Pamoja na mambo mengine, Bw. Mshomba amempongeza Mhe. Dkt. Tulia kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464