MKURUGENZI SHY DC AMESEMA PJT-MMMAM IMEKUJA TUBADILIKE KIFKRA

Mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Kisena Mabuba

Na Kareny Masasy,

PROGRAMU jumuishi ya Taifa  ya Makuzi na Malezi na  Maendeleo ya Awali ya mtoto  ( PJT-MMMAM ) ina lengo la kushughulikia mahitaji mahsusi  yaliyotambuliwa baada ya kufanya uchambuzi wa hali halisi ya huduma za program hiyo kwa watoto  wenye umri miaka 0 hadi minane (8).

Katika utambulisho wa programu ya PJT-MMMAM  iliyozinduliwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga  ambapo viongozi na wataalamu wa sekta mbalimbali walihudhuria.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga  kisena Mabuba akiwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo  anakasirishwa na baadhi ya wazazi kuwaachia watoto kwenda kwenye vibanda vya video nyakati za usiku wakati wakuangalia  mechi za mpira.

Mabuba anatoa ushuhuda anasema katika kibanda kimoja majira ya saa tano usiku hivi karibuni aliwakuta watoto wenye umri wa miaka sita wawili wakiwa wamechangamana na wakubwa wakiangalia  mechi za mpira zinazoendelea.

“Nilichukua jukumu la kuwakemea watoto hao nakutaka kufahamu wazazi wao  lakini nilikwenda moja kwa moja kwa  mhusika wa kibanda hicho nakumueleza  kuhusu watoto hao nikapiga marufuku  watoto nyakati za usiku”anasema Mabuba.

Mabuba anasema   suala la Malezi na Makuzi linamafundisho yake  kwa madhehebu ya dini kuna madrasa na sunday school na kila taasisi inatengeneza kupata misingi ya watoto waliokuwa kwenye hali ya utimilifu wa ukuaji na  kimaadili.

Mabuba anasema Siku hizi  jamii  ilivyo  sio  kama zamani kwani  imekuwa ikiona watoto ambao hawakuwazaa  haina haja ya kuwaangalia   bali ni mzazi mwenyewe  aliyezaa ndiyo jukumu lake.

“Msingi wa mradi huu ni  kufichua uovu na kutoa elimu katika  jamii na viongozi wa dini tusimame   pamoja tunaweza kuwaokoa watoto  kupitia  Programu  ya PJT-MMMAM hii  itunyanyue na itubadilishe kifikra”anasema Mabuba..

Mabuba anasema Taifa limeanza  kuchukua misingi ya malezi kwa watoto wote kwani linaapozungumziwa sula la malezi na makuzi  ni jambo kubwa kwa taifa haiwezekani  kuzingatia suala la malezi bora bila kusema lishe,afya,elimu , ulinzi na usalama.

Mwezeshaji  ambaye ni mratibu wa afya ya uzazi ya  mama, baba na mtoto  kutoka mkoani Shinyanga Halima Hamis anasema programu imekuja mahsusi kwa kuanzia   umri o hadi miaka nane.

Hamis anasema Makuzi na Maendeleo ya  Awali ya Mtoto yanaanzia tangu mtoto akiwa tumboni anazaliwa tayari ubongo wake unakuwa ukitambua  nakuzaliwa akiwa anajua  hivyo wasipowekeza  vizuri kwa watoto wanaweza kutengeneza taifa  lisilokuwa na watu timilifu.

“kwa mujibu wa  takwimu ya taifa  ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022  imeeleza  watoto wenye umri wa   kuanzia o hadi miaka nane  ni  zaidi  ya watoto takribani  16,000  hapa nchini   ambapo ni sawa na  asilimia 30 ya watanzania wote  hivyo kundi hili ni muhimu"anasema Hamis.

Hamisi anasema   yapo mambo mengi yanayopelekea kuwaathiri watoto kwani suala la malezi na makuzi ya watoto lazima ziangaliwe nguzo tano  ambazo ni Afya,Lishe,Malezi yenye mwitikio,Elimu au ujifunzaji wa awali  ikiwemo ulinzi na Usalama.

"Kuna mambo mengi yanatokea kuathiri ukuaji wa watoto kwani mtoto  akifanyiwa ukatili au kudhalilishwa kitendo hicho  kitaamuathiri hadi ukubwani nakushindwa kufanya majukumu yake kikamilifu”anasema Hamis.

.“Serikali imeona ipo changamoto  kwenye jamii kwa kufuata Mila na destruri zilizo mbaya kwani zipo nzuri ambazo  zinaweza kufuatwa ili kuweza kuwafikisha watoto katika ukuaji ulio timilifu”anasema Halima.

Ofisa ustawi wa jamii  kutoka mkoani Shinyanga Lyidia Kwesigabo anasema programu hii itakuwa endelevu inapaswa kuanza kutekelezwa kwenye kila sekta ambazo zimegusa watoto hawa kwa kubuni mikakati.

“Tukiangalia suala la elimu, afyalishe,Malezi yenye mwitikio  na ulinzi na usalama yote yanatuhusu tukishikamana kwa pamoja hakuna mtoto yoyote atakaye achwa nyuma na hili alilosema mkurugezi kuhusu watoto tuwalinde sote jamii nzima”anasema Kwesigabo.

Mchungaji wa kanisa la Angilikana lililopo kata ya Iselamagazi  Fanuel Shemtoi anasema yaliyoelezwa na mwezeshaji kupitia program ya PJT-MMMAM   yamemgusa nakusema alikuwa hafahamu ndiyo kwanza amepata darasa upya.

Shemtoi anasema alichogundua bado  jamii inaendekeza mila na desturi  katika malezi ya watoto wakifuata mgawanyiko wa majukumu katika familia ambapo baba amejikita kwenye utafutaji na ikifika jioni ndio kwenda kwenye vibanda vya mpira hawakai na watoto wao  kuwapa malezi yenye mwitikio.

“Suala la ulinzi na usalama wa mtoto linaachwa kwa mama pekee lakini hali hiyo imetokana na  jamii yenyewe kukosa elimu hii mapema hata kupitia  kanisani sasa tutaanza kutoa mahubiri kwa waumini wetu”anasema Shemtoi.

Diwani wa kata ya Iselamagazi Isack Sengerema anasema watoto wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili na watu wazima kuna tukio moja lilitokea hivi karibuni  la watoto  kulawitiwa  hivyo kupitia program hii jamii ikiielewa vizuri watoto watakuwa salama zaidi.

Baadhi ya wazazi wa kata ya Iselamagazi Musa Shija na Zawadi Moza  walipohojiwa  na mwandishi  kuwaruhusu watoto  nyakati za usiku kwenda kwenye vibanda vya video wanasema  ingawa wamekuwa wakiwafuata watu wazima ni makosa naona wanaingia nao kwa  kificho.


Wataalamu na baadhi ya viongozi wa kwenye jamii  wakiwa kwenye uzinduzi wa   PJT-MMMAM

Wataalamu mbalimbali  wa halmashauri  ya wilaya ya Shinyanga

Mkurugenzi wa halmashauri  ya wilaya ya Shinyanga  Kisena Mabuba.

Afisa  ustawi wa  Jamii kutoka mkoani Shinyanga  Lyidia Kwesigabo akitoa maelekezo katika kikao cha PJT-MMMAM

Wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga


Wataalamu wakisikiliza maelezo kutoka kwa mkurugenzi.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464