DC- Kishapu akiwa na wataalamu na viongozi wa dini
Na Kareny Masasy,
OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la ICS imetoa
utambulisho wa namna ya utekelezaji wa mpango wa Jumuishi wa Taifa Makuzi,Malezi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT MMMAM) kwa viomgozi
na wataalamu wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu pamoja na Ofisi ya Mkuu
wa Wilaya Kishapu ili waweze kuwafikisha watoto kwenye
ukuaji timilifu.
Akiwasilisha
programu hiyo leo Afisa ustawi wa jamii kutoka mkoani Shinyanga
Lyidia Kwesigabo alisema ili mtoto aweze kufikia hali nzuri ya ukuaji
bado ni lazima kusimamiwa kwenye nguzo tano ambazo ni Afya,Lishe bora,
Ujifunzaji wa awali,Malezi yenye mwitikio na ulinzi na Usalama.
Kikao
hicho kiliratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa
kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la investing in Children
and Strengtherning their Societies (ICS) nakuhudhuriwa na viongozi
pamoja na wataalamu wa idara mbalimbali ambapo Lydia Kwesigabo
alisema jamii inatakiwa ipate elimu hii muhimu kwa ujumuishi wake kwa
faida ya watoto familia na Taifa kwa ujumla.
Kwesigabo
amesema programu hiyo ilizinduliwa mwezi Desemba 2021 na ni programu ya
miaka mitano 2021/2022 hadi 2025/2026 ambayo imelenga watoto kuanzia
umri wa mwaka 0 hadi miaka ( 8) ambao ni umri uko katika hatua ya
ukuaji.
“Kwesigabo
amesema kuhusu dhana za ujifunzaji zinaweza kuandalliwa kulingana na
mazingira huskika kwa kutumia vitu vya asili na zikatumika katika vituo
vya Kulelea watoto wadogo mchana na shule za awali.
Kwesigabo
amesema nguzo zote 5 ni muhimu kwa watoto na pia mama anapokuwa
mjamzito hatakiwi kuwa na msongo wa mawazo na pia baba na mama
wanatakiwa wamsemeshe mtoto aliyeko tumboni kwani pia husaidia mtoto
kukua tumboni akiwa na furaha na uchangamshi mzuri na Ubungo kuendelea
kukua vizuri
Mgeni rasmi
ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amesema programu
hiyo ataisimamia vizuri hata kwenye ngazi za vijiji na kata kuhakikisha
watoto wanakuwa katika mazingira Bora.
"Kuna
baraza la madiwani kesho kutwa nitazungumza programu hiyo kwa madiwani
ili waweze kuuelewa na hakuna kitakacho shindikana watumia rasilimali
zilizopo kwenye maeneo Kama alivyosema afisa ustawi wa jamii"amesema
Mkude.
Mkurugenzi wa
halmashauri hiyo Emanuel Jonson amesema programu hiyo imekuja
wameipokea watatekeleza huku sheikhe kutoka Kishapu Adamu Nkhambi
alisema wanaume wanafikiri wakiweka ujauzito inatosha kumbe Kuna Malezi
zaidi yanahitajika ili mtoto aweze kukua vizuri na mwenye maadili.
Mwenyezi
Mungu katika vitabu vyake amesema kazaeni mjaze dunia tafsiri yake
kwenye Malezi wanaume na wanawake wawajibike utakuta mama anaenda
mwenyewe kliniki wakati wa ujauzito hadi anajifungua ,Malezi ya watoto
yukoi peke yake hivyo kama Viongozi wa Dini wataendelea kuelimisha
waumini wao juu ya programu hii
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akishika toleo la kitabu cha PJT-MMMAM.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Joseph Mkude akisikiliza utambulisho wa PJT-MMMAM
Sheikhe Adamu Nkhambi kutoka kishapu akichangia mada kuhusu PJT-MMMAM
Mkuu wa wilaya akiwa na viongozi wa dini.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464