Meneja msaidizi wa TRA mkoa wa Shinyanga Estomine Mosi akizungumza kwenye baraza la madiwani Kishapu
Suzy Butondo,Shinyanga press blog
Mamlaka ya Mapato Shinyanga TRA wametoa elimu ya ulipaji wa kodi kwa madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ambayo itawasaidia kujua kazi zinazofanywa na TRA na kutoa elimu kwa wafanyabiasha na wananchi katika maeneo yao ili waweze kujisajili na kulipa kodi.
Elimu hiyo imetolewa jana na afisa elimu na mawasiliano kwa mlipa kodi Semeni Mbeshi, kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Kishapu Mkoani hapa ambapo aliwaomba madiwani wote kuitumia elimu hiyo kuwaelimisha wananchi na wafanyabiashara wilayani humo.
Mbeshi akitoa elimu hiyo amesema TRA ni taasisi pekee imepewa mamlaka ya kukusanya kodi na kupeleke katika serikali kuu, inakagua listi kwenye maduka na inasimamia sheria za kodi, kwani hakuna maendeleo bila kodi, na chanzo kikubwa cha mapato ya serikali ni kodi, hivyo kila mfanya biashara ama mwekezaji anatakiwa kulipa kodi.
"Nchi inaweza kupata mkopo lakini chanzo kikuu ni kodi,ambayo inasimamia ujenzi wa miundombinu mbalimbali, huduma za kijamii sekta ya afya, elimu, barabara, na maji, hivyo ni vizuri wafanyabiashara watu wenye ajira na wawekezaji wakatoa kwa wakati kodi ili ziweze kufanya maendeleo"amesema Mbeshi.
Amesema sio kila mfanyabiashara anatakiwa kulipa kodi ni yule aliyefikia hatua ya kulipa kodi, ambaye ni mwenye mtaji wa milioni 4 na kuendelea ndiyo anatakiwa kulipa kodi, hivyo aliwaomba madiwani wakawaeleweshe wananchi kwani wengi wao hawaelewi ndiyo maana wamekuwa wakiona watu wa TRA wanafunga maduka na kukimbia.
"Pia tunawaomba waheshimiwa madiwani mkawaelimishe kwamba si kila mfanyabiashara anatakiwa kulipa kodi ni yule aliyefikia mapato ya milioni 4 na kuendelea ndiyo anatakiwa kulipa kodi , lakini kwa mujibu wa sheria mfanyabiashara wa kawaida ambaye hajafikia mtaji huo anatakiwa kuwa na TIN namba akiwa ni pamoja na kila mwananchi anatakiwa kuwa na TIN,"amesema Mbeshi
Mbeshi amesema mashine za EFD ni kifaa kinachotumika kutoa lisiti, kwa mfanyabiashara, na mwenye sifa ya kuitumia ni yule mwenye sifa ya kupata mauzo ya milioni 11 kwa mwaka ambaye ana uwezo wa kupata shilingi 11,000 kwa siku, na EFD ina faida kwa serikali kuifanya kutopoteza mapato na kwa mfanyabiashara inamsaidia kujua mwenendo wa biashara zake na kutoibiwa.
"Makosa ya kutotumia EFD mashine, mwaka. 2023 ukifanya kosa la kutotoa listi ilikuwa ni kutoa fane ya shilingi milioni 3 hadi shilingi milioni 4.5 na kwa ambaye hadai listi alikuwa akitozwa shilingi 30,000 hadi shilingi milioni 1,5 kwa mwaka huu 2024 sheria imebadilika usipotoa listi utalipa faini ya asilimia 20 ya mzigo wako uliouza, asiyedai listi asilimia 20 au shilingi 30,000,"amesema Mbeshi.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu Emmanuel Jonhson kodi ni kwa ajili ya wananchi wote, hivyo elimu hii ikasaidie kuwakumbusha wafanyabiashara na wananchi ili waweze kulipa kodi, wananchi wadai listi wanaponunua kitu na wananchi kujisajili kuwa na TIN namba kwani ni sheria iliyopitishwa na serikali.
Diwani wa kata ya Talaga Richard Dominick ameshukuru kwa kupata elimu hiyo lakini ameimba mamlaka hiyo kuandaa muda wa siku nzima ili waweze kutoa elimu ya kutosha waweze kuelewa vizuri na kuweza kuwapelekea wananchi wao.
Diwani wa kata ya Seke Bugiro Ferdinand Mpogomi ameshukuru kupata mafunzo hayo nakutoa ushauri kwamba wafike na maeneo ya chini kwa ajili ya kuwapatia elimu wahusika kwani wengi hawana uelewa wa kulipa kodi kudai listi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu William Jijimya halmashauri ya Kishapu inawafanyabiashara zaodi ya 3000 lakini haina ofisi ya TRA hivyo ni vizuri wakajenga ofisi ili waweze kukusanya mapato kwakaribu.
Naye meneja msaidizi wa TRA mkoa wa Shinyanga Estomine Mosi ambaye alimwakilisha Meneja wa TRA mkoa amesema ni kweli hawana ofisi za TRA ndiyo maana wameanza kutoa elimu ili waweze kuwaweka vizuri wafanyabiashara walipa kodi kikamilifu kwani mpaka sasa waliosajiliwa ni 1000 lakini wafanyabiashara wapo zaidi ya 3000 hivyo wafanyabiashara 2000 wote hawajajisajili.
"Suala la kujenga ofisi tutalifanyia kazi,lakini kwanza muwapelekee wananchi elimu hii ili waweze kujisajili, kwani idadi ya wafanyabiashara ikiongezeka tunaweza kujenga hoja ya kuweza kufungua ofisi Kishapu na wengi watakuwa na uelewa hawafunga maduka kwa kukimbia TRA,hivyo tunaomba ushirikiano wenu," amesema Mosi
Afisa elimu na mawasiliano kwa mlipa kodi Semeni Mbeshi,akitoa elimu ya kulipa kodi kwa madiwani wa halmashauri ya Kishapu
Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu Emmanuel Jonhson akozungu.za kwenye kikao cha baraza la madiwani
Viongozo wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha madiwani wa halmashauri ya Kishapu
Diwani wa Kata ya Talaga ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya uchumi Richard Dominick akizungumza kwenye kikao cha baraza hilo
Wakuu wa Idara kutoka sekta mbalimbali katika halmashauri ya Kishapu wakiwa kwenye baraza la madiwani
Madiwani wa halmashauro ya Kishapu na viongozi wa usamama wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani