Makundi mbalimbali na Wataalamu wa Manispaa Shinyanga
Na Kareny Masasy,Shinyanga
WATAALAMU wa Manispaa ya Shinyanga wameiahidi timu ya mkoa wakishirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Investing in Children and Strengthening their societies (ICS) juu ya utekelezaji wa Programu jumuishi ya taifa ya Makuzi ,Malezi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto( PJT-MMMAM).
Ambapo leo program hiyo imezinduliwa kwa Manispaa hiyo nakuhudhuriwa na makundi mbalimbali ikiwemo baadhi ya mashirika yanayotekeleza miradi ya afya na jamii huku mwezeshaji ambaye ni mratibu wa Elimu ya afya kwa umma mkoa Moses Mwita alitoa elimu juu ya nguzo tano zinazo mfanya mtoto kuwa katika ukuaji timilifu.
Naye Mratibu wa PJT MMMAM Mkoa Lydia Kwesigabo aliwapitisha washiriki juu ya mwongozo wa uratibu pamoja na viashiria ambabyo Halmashauri na Mkoa watakuwa wakipimwa navyo
Naye Afisa Mradi toka Shirika la ICS Lucy Maganga alieleza kuwa shirika linashughulika na masuala ya malezi katika mkoa litahakikisha linashirikiana na Mkoa pamoja na halmashauri na wadau wengine katika kuhakikisha lengo la PJT MMMAM linafikiwa
Ofisa Lishe manispaa ya Shinyanga Amran Mwakipesile amesema program hii imekuwa jumuishi hivyo wataitekeleza kwa ushirikiano huku Kaimu mganga mkuu wa Manispaa Charles Malogi akisema watahakikisha wanaifanya vizuri kwenye upande wa afya na ustawi wa jamii kupitia afua mbalimbali.
Mratibu wa chanjo manispaa ya Shinyanga Ramadhani Maneno amesema wao watatekeleza program hiyo sababu mara nyingi wamekuwa wakishughulika na watoto kuboresha afya zao kwa kupata chanjo za aina mbalimbali.
Mwenyekiti wa baraza la ushauri la Manispaa ya Shinyanga Stepheno Tano amesema program hiyo wameipokea huku akiahidi katika utendaji kazi kupitia baraza la wazee wataitambulisha PJT-MMMAM Ili wengine waweze kuifahamu zaidi.
Katibu wa bakwata wilaya ya Shinyanga Ramadhani Majani na Mwinjilisi wa kutoka kanisa la KKKT Kanoni Ndembezi Josephat wamesema program hiyo wataipeleka kwenye makundi waliyonayo yanayotoa elimu ya Malezi kwa wanawake na wanaume ili waifahamu na kutekeleza yanayowahusu kwa watoto.
Mwita amesema nguzo hizo zinatambuliwa kuwa ni Malezi yenye Mwitikio,lishe bora,afya, Ujifunzaji wa awali pamoja na Ulinzi na Usalama akielezea suala la lishe anasema mama mjamzito anatakiwa apate lishe iliyobora katika siku 1000 ili kumuweka mtoto katika afya nzuri.
“Ndiyo maana serikali inasisitiza halmashauri kutenga shilingi 1000 kwaajili ya lishe kwa mtoto baada ya kuona ipo changamoto kwenye jamii”anasema Mwita.
Mwita amesema wengi wamekuwa hawafahamu kuwa baba anatakiwa kuweka malezi yenye mwitikio kwa watoto wasiwaache kina mama peke yao na programu hiyo imelenga watoto kuanzia umri 0 hadi miaka nane.
Mratibu wa program hiyo mkoa ambaye ni ofisa Ustawi wa jamii Lyidia Kwesigabo amesisitiza suala la kuweka bajeti na mipango ya kila mwaka kwankuanzia na mwaka wa fedha 2024/25 shughuli za PJT MMMAM kwa sekta zote zinazo shughulika na mtoto.
Aidha Alisisitiza ujumuishaji wa agenda ya MMMAM katika vikao vya kisekta,Kamati za kudumu, vikao vya WDC na Baraza la madiwani
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464