Mkuu wa wilaya Mboni Mhita akielezea PJT-MMMAM
SERIKALI ya
mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na shirika lisilokuwa la kiserikali la
(ICS) limefanikisha katika uzinduzi wa programu jumuishi ya Taifa
ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM ) katika
halmashauri tatu za wilaya ya Kahama.
Halmashauri
hizo ni Msalala,Ushetu na manispaa ya Kahama ambapo uzinduzi huo
umefanyika kwa kila halmashauri huku mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita
akifungua rasmi program hiyo leo huku wakurugenzi wakipokea na
kuahidi kushirikiana katika utekelezaji.
Mboni
amesema programu hiyo imekuwa shirikishi ambapo imekuja kutatua
changamoto na kuboresha huduma za Malezi ya watoto kwa kuwa na nguzo tano
muhimu zilizoainishwa hivyo program hii itatoa uelewa mpana
na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha inasonga mbele.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Ushetu Hadija Kabojola amesema yeye ni mama nani mlezi
anafahamu umuhimu wa program hiyo ambayo inakwenda kumjenga mtoto ikisimamiwa
vizuri kwa ujumuishi ulivyo.
Mratibu wa Elimu ya afya kwa Umma Mkoa Moses Mwita ambaye alikuwa mwezeshaji amesema suala la ulinzi na usalama,ujifunzaji wa awali na malezi yenye mwitikio mfano mtoto anaposikia sauti ya kufokewa anajua au mtoto akiwa ananyonyeshwa huku mama akiwa hamjali inshara atakayo muonyesha ni kumng’ata.
zaidi kwa wazazi na jamii inayowazunguka wazazi wamekuwa hawashangai kuona watoto wao wakiwa wadogo kuzurura mtaa wapili bila kuwa na muangalizi.
Mratibu wa afya ya uzazi,mama,baba na mtoto mkoani Shinyanga Halima Hamis ambaye alikuwa mwezeshaji kuhusu program hiyo amesema kupitia sayansi ya elimu ya makuzi (SECD) inaonyesha mtoto anazaliwa akiwa na uelewa na kadri anavyokuwa ndivyo anavyoingiza kila kitu katika ubongo wake.
“Tusifanye
vitu kwa kusema huyu ni mtoto haelewi au kuongea lugha zisizo faa mbele yao
ndivyo anavyo nasa kwa kuona na kujifunza na kadri anavyokuwa katika
ubongo wake unanasa”anasema Halima.
Afisa ustawi wa jamii mkoa Lyidia Kwesigabo amesema program hii imekuja kuinarisha uratibu na mashirikiano katika kufanya kazi kwa ujumuishi na ushirikiano, aidha alieleza juu ya viashiria ambabyo kila halamshaui mpk mkoa utapimwa navyo hivyo ni jitihada zinatakiwa kila mmoja katika eneo lake kuhakiksha anatekeleza programy hii na elimu hii kuishusha kwenye ngazi za kata na vijiji au vitongoji ili jamii iweze kufikiwa.
Afisa Elimu
ya Watu Wazima Dedan Rutazka amesema mtoto anapoanzia tumboni
hadi miaka minane anatakiwa apate lishe ya kutosha ili hata mtoto akiwa
darasani apate uelewa wa kutosha huku Mratibu wa mradi wa Boost Fausta Luoga amesema
mwanafunzi anatakiwa apate chakula shuleni wazazi wahamasishwe wachangie na
walimu wapande mbogamboga shuleni.
Mganga mkuu
kutoka halmashauri ya Msalala Sisti Mosha amesema yote yaliyozungumzwa
kwenye program hiyo watakwenda kuyafanyia kazi hasa kupia kwenye idara ya
afya, ustawi wa jamii na lishe
Mchungaji Mapambano Sakobo pia mkurugenzi wa House of Hope kutoka Nyangalata Msalala amesema program hiyo imekuja na mambo mtambuka ambayo mengine yanaweza kutatuliwa na kutoa elimu zaidi kwa wazazi ili watoto wapate malezi mazuri yanayotarajiwa.
Ofisa
mipango kutoka halmashauri ya Ushetu Shigela Ganja nimefurahi
kwa kuunganishwa program hii ingependa maelekezo yatolewe namna ya ulaji
zipatikane mbogamboga shuleni ili kuelekeza kwenye lishe kwani ubongo wa mtoto
kwenye miaka 0 hadi minane inakuwa kwenye hatua ukuaji.
Mkuu wa
kitengo cha sheria kutoka Manispaa ya Kahama Stephen Magalla amesema
zimesemwa changamoto nyingi kwa watoto ambapo ipo sheria ya mtoto namba
21 ya mwaka 2009 ambayo inatumika ni kuhakikisha inasimamiwa vizuri ili
kuwaokoa watoto nay ale yote yaliyoelezwa yatasimamiwa.
Lucy Magnga
kutoka shirika la ICS amewaeleza wataalamu,viongozi wa dini na
makundi ya kijamii kuwa wao kuungana na serikali ni kutokana na shirika
hilo kushughulikia masuala ya malezi ya watoto nakuwataka kushiriki vyema
programu hiyo ili kumkomboa mtoto