Header Ads Widget

SHINYANGA WAMUOMBEA DUA NA SALA,RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI TANZANIA HAYATI ALI HASSAN MWINYI APUMZIKE KWA AMANI

SHINYANGA WAMUOMBEA DUA NA SALA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI TANZANIA HAYATI ALI HASSAN MWINYI APUMZIKE KWA AMANI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
WANANCHI kutoka Madhehebu Mbalimbali ya kidini mkoani Shinyanga, wamemuombea Dua na Sala Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Nchini Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi apumzike kwa Amani.

Maombi hayo yamefanyika leo Marchi 4 kwenye Viwanja vya Sabasaba Manispaa ya Shinyanga huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Mndeme akizungumza kwenye maombi hayo, kwanza amewashukuru wananchi wa Shinyanga kutoka Madhebu mbalimbali kujitokeza kumuombea Rais Mstaafu Hayati Ali Hassani Mwinyi apumzike kwa Amani, na kuahidi kwamba watayaenzi yale mema ambayo amewaachia.

“Tumekusanyika hapa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kutoka Madhehebu mbalimbali ili tumombee Dua na Sala Rais wetu Mstaafu Hayati Ali Hassan Mwinyi ili Mwenyezi Mungu ampokee katika Ufalme wake na ampatie pumziko la Amani,”amesema Mndeme.
“Tumuombee pia Rais Wetu Samia Suluhu Hassan kwa Msiba huu Mzito ambao ameupata kwa kuondokewa na kiongozi Mkubwa ambaye alikuwa akimtegemea pia katika ushauri mbalimbali namna ya kuongoza nchi na kuwatumikia Watanzania,”ameongeza Mndeme.

Aidha, aliitakia pia pole Familia yote ya Marehemu Hayati Ali Hassan Mwinyi pamoja na Wajane ambao wameachwa kwamba Mwenyezi Mungu awapatie faraja katika kipindi hiki kigumu ambacho wameondokewa na mpendwa wao.
Katika hatua nyingine Mdeme, amewakaribisha Wananchi wa Shinyanga na viongozi mbalimbali, kwamba wafike kwenye Ofisi za Mkoa huo Kusaini Kitabu cha Maombolezo

Naye Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya, akizungumza kwenye Maombi hayo, amesema katika Mkoa huo hawata msahau Rais Mwinyi kwa kutatua Mgogoro Mkubwa ambao ulikuwapo wa kiimani, ambapo aliutatua na kudumisha Amani.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili nchini Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi alifariki dunia Februari 29 mwaka huu akiwa na miaka 98 alipokuwa akipatiwa Matibabu katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam na amezikwa Marchi 2, 2024 huko Unguja.

Na alikuwa Rais wa Pili wa Tanzania kuanzia mwaka 1985 hadi 1995, Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe Amina.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa na viongozi wa dini kwenye Maombi ya kumuombea Dua na Sala Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi apumzike kwa Amani.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye, maombi ya kumuombea Dua na Sala Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi apumzike kwa Amani.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye maombi ya kumuombea Dua na Sala, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi apumzike kwa Amani.
Kiongozi wa dini ya Kikristo akiongoza Sala ya kumuombea Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi ampumzike kwa Amani.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akiongoza Dua ya kumuombea Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania Ali Hassan Mwinyi apumzike kwa Amani.
Dua ya kumuombea Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania Ali Hassan Mwinyi ikiendelea.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Dua na Sala ya kumuombea Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi ampumzike kwa Amani.
Wanafunzi kutoka Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM)wakiwa kwenye Dua na Sala ya kumuombea Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi ampumzike kwa Amani.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye Dua na Sala ya kumuombea Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi ampumzike kwa Amani.

Post a Comment

0 Comments