MGODI WA ALMASI MWADUI,HALMASHAURI YA KISHAPU WATIA SAINI HATI YA MAKUBALIANO UTEKELEZAJI MIRADI YA CSR SH.BILIONI 1


MGODI WA ALMASI MWADUI,HALMASHAURI YA KISHAPU WATIA SAINI HATI YA MAKUBALIANO UTEKELEZAJI MIRADI YA CSR SH.BILIONI 1

Na Marco Maduhu,KISHAPU
MGODI wa Madini ya Almasi Mwadui Williamson Diamond (WDL)pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, wametia Saini hati ya makubaliano (MoU)ya utekelezaji wa Miradi 16 ya Maendeleo kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) Sh.Bilioni 1.
Utiaji Saini huo umefanyika leo Marchi 6,2024 Katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo wanatoka kwenye vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi huo.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude,akizungumza wakati wa kufungua hafla ya Utiaji Saini, ameupongeza Mgodi wa Mwadui kwa kutoa fedha hizo za CSR, ambazo zitatumika kutekeleza Miradi Mbalimbali ya Maendeleo kwa wananchi.
Amesema Mwaka Jana Mgodi huo ulitoa tena fedha za CSR Sh.bilioni 1.2 ambayo ilitekeleza Miradi Mbalimbali ya Maendeleo,na Mwaka huu wametoa tena Sh.bilioni 1 ambayo itatekeleza Miradi 16 ya Maendeleo.

"Fedha hizi zinakwenda kutekeleza Miradi ya Maendeleo ambayo inaigusa Jamii, sababu imeibuliwa na wananchi wenyewe ikiwamo ya Sekta ya Afya,Elimu,Miundombinu ya Stendi na Barabara,"amesema Mkude.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu William Jijimya, amesema fedha hizo Sh.bilioni 1 kwamba asilimia 60 zitatekeleza Miradi ya kimkakati, na Asilimia 40 zitakeleza Miradi ya Maendeleo katika Vijiji 12 ambavyo vinazunguka Mgodi wa Mwadui.

Naye Afisa Uhusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo, amesema wametekeleza Takwa la Kisheria kwa kutoa fedha hizo za CSR Sh.bilioni 1 ikiwa ni asilimia 0.7 ya pato ghafi.
Aidha,ameiomba Serikali wakiwamo na Viongozi kutoka Vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi, kwamba waimalishe ulinzi na kuzuia uvamizi ndani ya Mgodi huo ili wasije kusitisha uzalishaji, bali waendelee na uzalishaji hali ambayo itaongeza mapato ya CSR.

Amewataka pia Wananchi ambao wanatekelezewa Miradi hiyo ya Maendeleo kwenye maeneo Yao kwamba waitunze ili itumike vizazi na vizazi.
Mwenyekiti wa Vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi wa Almasi Mwadui Charles Manyenye, ameupongeza Mgodi huo kwa kuendelea kutoa fedha za CSR ambazo zimeendelea kuimarisha Mahusiano Mazuri Kati ya Wananchi na Mgodi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye Hafla ya utiaji Saini Hati ya Makubaliano ya Utekelezaji wa Miradi ya CSR kati ya Mgodi wa Mwadui na Halmashauri ya Kishapu.
Mwenyekiti wa Halmashuri ya wilaya ya Kishapu Wiliam Jijimya akizungumza kwenye Hafla ya utiaji Saini Hati ya Makubaliano ya Utekelezaji wa Miradi ya CSR kati ya Mgodi wa Mwadui na Halmashauri ya Kishapu.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu akizungumza kwenye Hafla ya utiaji Saini Hati ya Makubaliano ya Utekelezaji wa Miradi ya CSR kati ya Mgodi wa Mwadui na Halmashauri ya Kishapu.
Afisa Uhusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo akizungumza kwenye hafla hiyo.
Diwani wa Maganzo Mbaru Kidiga akizungumza kwa niaba ya Madiwani ambao wanazungukwa na Mgodi wa Almasi Mwadui kwenye Hafla hiyo ya Utiaji Saini Hati ya Makubaliano ya Utekelezaji wa Miradi ya CSR kati ya Mgodi wa Mwadui na Halmashauri ya Kishapu.
Mwenyekiti wa Vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi wa Mwadui Charles Manyenye akizungumza kwenye Hafla hiyo ya Utiaji Saini Hati ya Makubaliano ya Utekelezaji wa Miradi ya CSR kati ya Mgodi wa Mwadui na Halmashauri ya Kishapu.
Utiaji Saini Hati ya Makubaliano ya Utekelezaji wa Miradi ya CSR ukiendelea baina ya Mgodi wa Mwadui na Halmashauri ya Kishapu.
Utiaji Saini Hati ya Makubaliano ya Utekelezaji wa Miradi ya CSR ukiendelea baina ya Mgodi wa Mwadui na Halmashauri ya Kishapu.
Utiaji Saini Hati ya Makubaliano ya Utekelezaji wa Miradi ya CSR ukiendelea baina ya Mgodi wa Mwadui na Halmashauri ya Kishapu.
Utiaji Saini Hati ya Makubaliano ya Utekelezaji wa Miradi ya CSR ukiendelea baina ya Mgodi wa Mwadui na Halmashauri ya Kishapu.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Afisa Uhusiano Mgodi wa Mwadui Benard Mihayo (kulia) wakishikana Mikono ya Pongezi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu Wiliam Jijimya mara baada ya kusaini hati ya Makubaliano Fedha za CSR.
Maafisa kutoka Mgodi wa Almasi Mwadui wakiwa kwenye hafla hiyo.
Madiwani kutoka Kata ambazo zinazunguka Mgodi wa Mwadui wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wenyeviti wa Vijiji ambavyo vinazunguka Mgodi wa Almasi Mwadui wakiwa kwenye hafla hiyo.
Watendaji kutoka Vijiji 12 ambavyo vinazunguka Mgodi wa Mwadui wakiwa kwenye hafla hiyo.
Hafla ya Utiaji Saini ikiendelea.
Hafla ya Utiaji Saini ikiendelea.
Hafla ya Utiaji Saini ikiendelea.
Hafla ya Utiaji Saini ikiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464