RC MNDEME AMEAGIZA WAFANYABIASHARA WANAOENDELEA KUFICHA SUKARI WAKAMATWE NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI, 9 WADAKWA


RC MNDEME AMEAGIZA WAFANYABIASHARA WANAOENDELEA KUFICHA SUKARI WAKAMATWE NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI, 9 WADAKWA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amewaagiza Wakuu wa wilaya mkoani humo, kwamba watumie mbinu zote pamoja na vyombo walivyonavyo, kuwasaka Wafanyabiashara ambao bado wanaendelea kuficha Sukari pamoja kuuza kinyume na bei elekezi ya Serikali na kuwachukulia hatua ikiwamo kuwafikisha Mahakamani.
Mndeme ametoa Maagizo hayo leo Marchi 7,2024 kwenye Kikao cha Kamati cha Ushauri ya Mkoa wa Shinyanga RCC.

Amesema Mkoa wa Shinyanga bado unakabiliwa na tatizo la Sukari, ambapo kuna baadhi ya Wafanyabiashara wamekuwa wakificha Sukari pamoja na kuuza kwa bei isiyo elekezi ya Serikali na kuwaumiza wananchi.
“Wakuu wa wilaya tumieni mbinu yoyote na vyombo mlivyonavyo kuhakikisha mnawasaka na kuwachukulia hatua Wafanyabishara ambao wamekuwa wakificha Sukari pamoja na wale ambao wanauza kinyume na bei elekezi ya Serikali, wakamate na kuwafikisha Mahakamani,”amesema Mndeme.

“Sasa hivi tunaelekea kwenye Mfungo wa Ramadhani hivyo kuendelea kuficha Sukari na kuuza kwa bei isiyo elekezi siyo sawa, bali tunawataka Wafanyabiashara wawe Wazalendo, wawe na Utu, na watii Maagizo ya Serikali, na mpaka sasa tumesha wakamata Wafanyabiashara Tisa wa Sukari,”ameongeza Mndeme.
Aidha, amesema bei elekezi ya Rejareja Mwananchi anapaswa kuuziwa Sukari Kilo moja Sh. 2800, lakini anauziwa Sh.3,000 hadi 5,000.

Amewaagiza pia Wataalamu wa Kilimo kupima hali ya udogo ili kubaini Mabonde ambayo yatafaa kwa Kilimo cha Miwa ili kijengwe Kiwanda cha Sukari, ili kukabiliana na upungufu wa Sukari ndani ya Mkoa.

Katika hatua nyingine amezungumzia Mlipuko wa Ugonjwa wa Kipindupindu na kubainisha kwamba kati ya Watu 216, waliripotiwa, kwamba 127 walibainika kuwa na Vimelea vya Kipundupindu, huku Watu Sita wakifa kutokana na Ugonjwa huo.
Amesema Ugonjwa huo wa Kipindupindu kwa sasa umeshika kasi Manispaa ya Shinyanga hasa katika Kata ya Ndala na Kambarage, na kutoa maelekezo kwa Wataalamu wa Afya watoe elimu kwa wananchi kuzingatia kanuni za Afya, pamoja kufuatilia Usafi katika Maeneo ya Masoko na uuzaji wa vyakula.

Pia Mkuu wa Mkoa ameziagiza Halmashauri zote za Mkoa huo kutenga maeneo kwa ajili ya ufugaji, ili kuongeza uzalishaji wa mifugo.
Akizungumzia upande wa huduma za Maji, amesema Rais Samia katika Utawala wake ametoa Sh.bilioni 500 ya fedha za Maji na kuna Miradi mipya ya Maji 47 ambayo inaendelea kutekelezwa ili kuongeza Mtandao wa Maji na kuagiza yanapofanyika Matengenezo ya maji yafanyike kwa ubora zaidi.


Kwenye kikao hicho zimewasilishwa na kujadiliwa taarifa Mbalimbali ikiwamo ya Bajeti ya Mkoa,Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA)Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Sekta ya Umeme, Kilimo pamoja na Taarifa za Maji.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye kikao cha RCC.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof; Siza Tumbo akizungumza kwenye kikao cha RCC.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza kwenye kikao hicho cha RCC.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu akizungumza kwenye kikao hicho cha RCC.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464