Header Ads Widget

RC MNDEME AMEWATAKA WANAWAKE SHINYANGA WAJIEPUSHE NA MIKOPO KAUSHA DAMU,MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

RC MNDEME AMEWATAKA WANAWAKE SHINYANGA WAJIEPUSHE NA MIKOPO KAUSHA DAMU,MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme,ameongoza Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani mkoani humo, huku akiwatahadharisha wanawake wajiepushe na mikopo kausha damu ambayo inawarudisha nyuma kiuchumi.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Marchi 8, 2024 katika Viwanja vya Sabasaba Manispaa ya Shinyanga.
Mndeme akizungumza kwenye Maadhimisho hayo amewataka Wanawake mkoani humo wawe wavumilivu katika kipindi hiki cha Mpito, ambapo Serikali inaendelea kufanya Maboresho juu ya utoaji wa Mikopo asilimia 10 na wasijiingize kwenye mikopo kausha damu.

“Mnamo mwezi Aprili 2023 Serikali ilisitisha utoaji wa mikopo asilimia 10 ya Mapato ya ndani ya halmashauri kwa makundi ya Wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu, na ilisitisha kwa lengo Mahususi la kuboresha utoaji wa mikopo hii, na pia kufuatilia marejesho ya mikopo ili kuhakikisha mzunguko unakuwa endelevu,” amesema Mndeme.
“Mkoa unaendelea kusubili maelekezo na utaratibu mpya wa utoaji wa mikopo hii ya asilimia 10, hivyo tuwaombe wanawake muwe na subira katika kipindi hiki cha mpito, na mjiepushe na mikopo kausha damu ambayo inarejesha nyuma jitihada za kujikwamua kiuchumi,”ameongeza.

Aidha,Mndeme ametoa Maagizo kwa kwa Wakuu wa Wilaya Mkoani humo, kwamba wasimamie uanzishaji wa Majukwa ya Wanawake Kiuchumi kuanzia ngazi ya Kata, sababu yanawaimarisha wanawake na kuwapa nguvu pamoja na kuinuka kiuchumi.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa, amempongeza Rais Samia kwa kuwa amini Wanawake na kuwapatia fursa mbalimbali za uongozi, na wamewakuwa wakifanya vizuri kwa kuiga uongozi wake na kuwatumikia wananchi katika kuwaletea maendeleo.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba naye amempongeza Rais Samia, kwa kuwaamini wanawake na kuwapatia nasafi mbalimbali za uongozi, na wamekuwa wakifanya vizuri kwenye utendaji wao kazi.
Naye Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Christina Mzava, amewataka wanawake wajikite pia kwenye Malezi ya Watoto ili kuzuia Momonyoko wa Maadili.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Shinyanga Grace Bizulu, amewataka wanawake katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu kwamba wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi za uongozi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi, amewahakikishia Wanawake mkoani humo, kwamba Jeshi hilo limejipanga vyema kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake kiuchumi Mkoa wa Shinyanga Rejina Malimi, amempongeza Rais Samia kwa kuasisi Jukwaa hilo, ambalo limekuwa chachu ya kuwainua wanawake kiuchumi.
Ameiomba pia Serikali kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wanawake, likiwamo tatizo la mikopo kausha damu, Mila na desturi Kandamizi, pamoja na Vitendo vya ukatili.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani mwaka huu inasema”Wekeza kwa Wanawake,Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii,”

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Christina Mzava akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Christina Mzava akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga Grace Bizulu akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Shinyanga Regina Malimi akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akipokea zawadi Mchele Kilo 10 kutoka kwa Wanawake wa Ushetu
Wanawake wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoani Shinyanga
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga yakiendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akipokea Mifuko ya Saruji 31 kutoka kwa Mtandao wa Wanawake wa Jeshi la Polisi, kwa ajili ya ujenzi wa Bweni Kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga cha kulea watoto wenye uhitaji.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akikabidhi chakula kwa ajili ya watoto ambao ni Wahanga wa Ukatili katika Kituo cha Agape.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akitembelea Mabanda kwenye Maadhimisho hayo ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga, akiwa katika Banda wa VETA.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiwa katika Banda la Women For Change katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Shinyanga.
Awali Wanawake wakiwa katika Mandamano.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.

Post a Comment

0 Comments