Header Ads Widget

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA UJENZI WA MKONGO WA TAIFA TTCL SHINYANGA


KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA UJENZI WA MKONGO WA TAIFA TTCL SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu,imetembelea ujenzi wa Mkongo wa Taifa katika Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Shinyanga, na kuipongeza Serikali kwa uwekezaji huo.
Ziara hiyo imefanyika leo Marchi 14,2024.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Seleman Kakoso, amesema kutokana na Uwekezaji mkubwa ambao umefanyika juu ya ujenzi wa Mkongo huo wa Taifa, kwamba ni wakati sasa umefika wa Shirika la TTCL kujiendesha kibiashara.
“Tunaipongeza Serikali kwa uwekezaji huu mkubwa, kupitia Mkongo wa Taifa ambapo mtaingiza fedha nyingi sana ndani na nje ya nchi, hivyo mnapaswa kujiendesha sasa kibiashara,”amesema Kakoso.

Ameitaka pia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,kwamba wawe wabunifu pamoja na kuja na mawazo ya nchi ya Tanzania iwe na “Sitelite” yake yenyewe ili kuimarisha Mfumo wa Teknolojia.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, amesema ujenzi huo wa Mkongo wa Taifa upo katika wakati wake ambapo kwa sasa dunia inakwenda kwenye uchumi wa Kidigitali.

Mtendaji Mkuu wa TTCL Peter Ulanga akisoma taarifa ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa kwa Kamati hiyo, amesema mwaka wa fedha 2023/2024 Wizara hiyo ilitengewa fedha Sh.bilioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa Kilomita 1,600 na Vituo 32 vya Mkongo wa Taifa pamoja na kufanya upanuzi wa njia za usafirishaji wa mawasiliano kutoka 800 Gbps kwenda 2000 Gbps.
Amesema pia wanafanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Vituo vya kutunzia Taarifa (Data Center)Zanzibar na Dodoma na kuunganisha Taasisi 50 kwenye Mkongo wa Taifa, pamoja na kuunganisha nchi ya Kidemokrasia ya Kongo.

“Awamu ya kwanza ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa ilianza mwaka 2009 ikiwa na uwezo wa 40G na baadae kuongezwa uwezo kuwa 200G hadi 400G kwa Singida,Shinyanga na Mwanza,”amesema Ulanga.
Aidha, amesema ujenzi wa Mkongo wa Taifa mkoani Shinyanga umejikita katika katika Maeneo Makuu Mawili ambayo ni Usimikaji wa Mitambo na Ujenzi wa Nguzo za Zege sambamba na uvutaji wa Waya za Faiba.

“Katika Awamu hii uwezo wa Mitambo umeongezwa kutoka 200G mpaka 800G na tayari Mitambo inafanya kazi kwa Singida, Shinyanga,Mwanza na ujenzi unaendelea katika maeneo mengine,”ameongeza Ulanga.
Pia amebainisha Changamoto ambazo zilikuwa zikikwamisha ujenzi wa Mkongo huo wa Taifa ambazo tayari wameshazifanyia utatuzi, kwamba ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutozima Umeme kwa wakati ili kupisha ujenzi huo, sababu Usimikaji wa Nguzo za Zege na uvutaji wa Waya wa Faiba unafanyika sambamba na Njia za Waya za Umeme.


Amebainisha Changamoto nyingine kuwa ni Mvua kuwa nyingi na kusababisha Mazingira ya kufanya kazi kuwa Magumu.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Seleman Kakoso akizungumza kwenye ziara TTCL Shinyanga.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza kwenye ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu TTCL Shinyanga.
Mtendaji Mkuu wa TTCL Peter Ulanga akitoa taarifa ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiwa ziara TTCL Shinyanga.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiwa ziara TTCL Shinyanga.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiwa ziara TTCL Shinyanga.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiwa ziara TTCL Shinyanga.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiwa ziara TTCL Shinyanga.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakipiga picha ya pamoja TTCL Shinyanga.

Post a Comment

0 Comments