KAMATI YA BUNGE PAC YAPONGEZA UWEKEZAJI MKUBWA KIWANDA CHA BOMBA LA MAFUTA GHAFI “EACOP” SOJO-NZEGA
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imetembelea kuona uwekezaji mkubwa wa Kiwanda cha kuweka Mifumo ya upashwaji Joto Mafuta, itakayozuia upotevu wa Joto kwenye Mabomba yatakayotumika kwenye mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima Uganda hadi Tanga Chongoleani, kilichopo Kijiji cha Sojo wilayani Nzega.
Ziara hiyo imefanyika leo Marchi 19, 2024.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Japhet Hasunga,akizungumza kwenye ziara hiyo ameipongeza Serikali ya Tanzania pamoja na Uganda kwa Uwekezaji huo Mkubwa wa Bomba la Mafuta Ghafi ambalo litachochea uchumi Wanchi zote mbili.
Amesema Kazi ya Kamati hiyo ni kufuatilia fedha za Umma ambazo ziliidhinishwa na Bunge juu ya utekelezaji wa Mradi huo,ili kuona thamani yake na tija wa mradi huo, ambapo wameona mafanikio makubwa ikiwamo wananchi kupata ajira pamoja na kujengewa nyumba zuri za ulipwaji fidia.
“Kamati ya PAC inaipongeza Serikali ya Tanzania pamoja na Uganda kwa Uwekezaji huu Mkubwa wa Bomba la Mafuta Ghafi ambalo litachochea ukuaji wa uchumi wanchi zote mbili, pamoja na kupunguza Kiwango cha Umaskini kwa wananchi,”amesema Hasunga.
“Ziara yetu hii ilikuwa ni kuona Maendeleo ya Ujenzi wa Kiwanda hiki na tumeshuhudia Uwekezaji Mkubwa sana na tumeridhika na Uwekezaji huu sababu una Tija na fedha zimetumika vizuri,”ameongeza.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mussa Makame, amesema Kiwanda hicho kwa sasa ujenzi wake upo asilimia 6, na Marchi 26 mwaka huu Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati atakizindua.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mussa Makame akizungumza kwenye ziara hiyo ya Kamati ya PAC kwenye Kiwanda hicho.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya PAC Japhet Hasunga akizungumza kwenye ziara hiyo.
Mwakilishi wa Ujenzi wa Kiwanda hicho (Site Representative) Guillaume Mallevaey akizungumza kwenye ziara hiyo ya Kamati ya PAC.
Wajumbe wa Kamati ya PAC wakiwa ziara kwenye Kiwanda hicho.
Wajumbe wa Kamati ya PAC wakiwa ziara kwenye Kiwanda hicho.
Wajumbe wa Kamati ya PAC wakiwa ziara kwenye Kiwanda hicho.
Wajumbe wa Kamati ya PAC wakiwa ziara kwenye Kiwanda hicho.
Wajumbe wa Kamati ya PAC wakiwa ziara kwenye Kiwanda hicho.
Mabomba ya Mafuta Ghafi yakiwa eneo la Mradi.
Mabomba ya Mafuta Ghafi yakiwa eneo la Mradi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464