SAVE THE CHILDREN,RAFIKI SDO WAMEWAJENGEA UWEZO WA KUJIAMINI MABARAZA YA WATOTO KUSHIRIKI KWENYE VIKAO VYA MAAMUZI NA KUTOA MAONI YAO
SHIRIKA la Save The Children pamoja na Rafiki SDO, wametoa Mafunzo kwa Mabaraza ya watoto kwa shule za Msingi na Sekondari Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga, kwa kuwajengea uwezo wa kujiamini na kushiriki kwenye vikao mbalimbali vya maamuzi na kutoa maoni au mapendekezo ambayo ni mahitaji ya watoto.
Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza kutolewa leo Marchi 15, 2024 na Mashirika hayo kwa ufadhili wa Shirika la Sida.
Afisa Miradi kutoka Shirika la Save The Children Victor Mkiza, akizungumza kwenye mafunzo hayo, amesema watoto kupitia Mabaraza yao, wanapaswa kuwa wanashirikishwa na watoa maamuzi kwenye vikao, hasa kwa masuala ambayo yanahusu maslahi ya watoto ili wawe wanatoa maoni na mapendekezo yao.
Amesema Mtoto akishirikishwa kwenye vikao kwa masuala yanayowahusu, itakuwa ni virahisi kujua vipaumbele vyao ambavyo wanahitaji kutekelezewa katika mipango ya Serikali, kuliko kujiamulia na kuwatekelezea vitu ambavyo siyo mahitaji yao.
“Mtoto anahaki ya kushirikishwa kwenye vikao mbalimbali vya maamuzi kwa masuala yanayowahusu, ili watoe maoni au mapendekezo na kutekelezewa vipaumbele vyao,”amesema Mkiza.
“Juzi na Jana tumetoa Mafunzo kwa watoa maamuzi namna ya kushirikisha watoto kwenye vikao mbalimbali kwa masuala ambayo yanahusu watoto, na leo tumewaita watoto kupitia Mabaraza yao ili kuwajengea uwezo wa kujiamini watakapokuwa wakishirikishwa kwenye vikao hivyo watoe mapendekezo yao na kufanyiwa kazi,”ameongeza.
Meneja Mradi wa Azaki kuimarisha Mabaraza ya Watoto (MKUA) kutoka Shirika la Rafiki SDO Maria Maduhu, amesema Mafunzo hayo ni ya muhimu kwa watoto katika kuwajengea uwezo wa kushiriki kwenye vikao mbalimbali vya maamuzi kwa masuala yanaoyohusu maslahi ya watoto na kutoa mapendekezo yao.
Nao baadhi ya watoto wamesema, ushirikishwaji watoto kwenye vikao mbalimbali vya maamuzi hasa kwa masuala yanoyahusu, itasaidia kutatua matatizo yao na kuzifikia ndoto zao, huku wakisema kwamba mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kujiamini hasa wanapokutana na viongozi kwenye vikao na kutoa maoni yao.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Meneja Mradi wa (MKUA) kutoka Rafiki SDO Maria Maduhu, akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Afisa Miradi kutoka Shirika la Save The Children Victor Mkiza, akitoa mafunzo hayo kwa Mabaraza ya Watoto ngazi ya Kata ya Ngokolo kwa shule za Msingi na Sekondari.
Afisa Miradi kutoka Shirika la Save The Children Victor Mkiza, akiendelea kutoa mafunzo hayo kwa Mabaraza ya Watoto ngazi ya Kata ya Ngokolo kwa shule za Msingi na Sekondari.
Afisa Miradi kutoka Shirika la Save The Children Victor Mkiza, akiendelea kutoa mafunzo hayo kwa Mabaraza ya Watoto ngazi ya Kata ya Ngokolo kwa shule za Msingi na Sekondari.
Afisa Ufutailiaji na Tathimini kutoka Rafiki SDO Sospeter Ayieko akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Ufutailiaji na Tathimini kutoka Rafiki SDO Sospeter Ayieko akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Wajumbe wa Mabaraza ya watoto wakiwa kwenye kazi za Vikundi.
Wajumbe wa Mabaraza ya watoto wakiendelea na kazi za Vikundi.
Wajumbe wa Mabaraza ya watoto wakiendelea na kazi za Vikundi.
Wajumbe wa Mabaraza ya watoto wakiendelea na kazi za Vikundi.
Wajumbe wa Mabaraza ya watoto wakiendelea na kazi za Vikundi.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464