Header Ads Widget

JENGO JIPYA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA SHINYANGA LAFUNGULIWA RASMI

JENGO JIPYA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA SHINYANGA LAFUNGULIWA RASMI

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dk.Khatibu Kazungu,amefungua Rasmi Jengo Jipya la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga.
Hafla ya ufunguzi wa Jengo hilo imefanyika leo Marchi 16,2024 ikiwa ni sambamba na ufunguzi wa Majengo Mengine Matano ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kutoka Mikoa Pwani,Manyara,Katavi, Rukwa na wenyeji Shinyanga.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, amesema ujenzi wa Majengo hayo ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, ni kuongeza tija katika utoaji wa huduma kwa wadau na wananchi katika Mnyororo mzima wa haki Jinai.
"Tunampongeza Rais Samia kwa kuleta Mageuzi katika Sekta ya haki Jinai,hivyo Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kupitia Majengo haya mtaongeza ufanisi katika utendaji kazi wenu pamoja na kutoa haki kwa wananchi na kwa wakati," amesema Dk.Kazungu.

"Utoaji wa haki kwa usawa ni kupunguza Malalamiko katika Jamii,hivyo fanyeni kazi zenu kwa Maadili, na weledi,”ameongeza.
Pia ameitaka Ofisi hiyo ya Taifa ya Mashtaka kuendelea kuweka mikakati ya kukamilisha ujenzi wa Ofisi katika Mikoa na Wilaya zilizobaki pamoja na kufanya maboresho kwenye maeneo mengine kama vile maslahi ya Watumishi, pamoja na kuendelea kushirikiana na Vyombo na Taasisi zilizopo kwenye Mnyororo wa utoaji wa haki jinai.

Naye Mkurugenzi Mkuu Mashtaka (DPP)Sylvester Mwakitalu, amesema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ilianzishwa mwaka 2018 kufuatia mabadiliko ya Muundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, na kwamba Muundo wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaelekeza kuwepo kwa Ofisi za Mashtaka kwa Mikoa yote na Wilaya.
Amesema baadhi ya Mikoa na wilaya wameshajenga Ofisi za Taifa za Mashtaka na Mikoa mingine wamepanga Ofisi, na kwamba mwaka wa fedha ujao wametengewa tena fedha za Maendeleo, na watajenga Ofisi 3 ili kuendelea kusogeza huduma kwa wananchi.

“Tukiwa na Majengo ya Ofisi zetu za Taifa za Mashtaka tutafanya kazi kwa uhuru zaidi na hata faragha kwa wateja wetu itaongezeka, kuliko kufanya kazi kwenye Majengo ya kupanga na wakati mwingine Ofisi inakuwa ndogo mnakosa usiri,”amesema Mwakitalu.
“Ofisi ya Taifa ya Mashtaka inapaswa kuwa na Mejengo ya Ofisi 169 katika Mikoa na Wilaya zote nchini, hadi sasa Ofisini ina Majengo 7 ambayo yapo Mikoa ya Iringa, Ilala-Pwani, Manyara, Katavi, Rukwa na wilaya ya Serengeti na tunaupungufu wa Majengo 161 ukiondoa Jengo la Makao Makuu,”ameongeza.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali, amesema Ofisi hiyo mpya ya Taifa ya Mashtaka wanategemea ufanisi wa kazi utaongezeka pamoja na kupata hadithi nzuri za Mashtaka Mahakamani zisizo na ukakasi, huku akiomba Ofisi kama hiyo ijengwe pia na Mkoa wa Simiyu.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Joseph Mkude ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu, amepongeza ujenzi wa Jengo la Ofisi hiyo ya Taifa ya Mashtaka. Huku akimpongeza Rais Samia kwa kuwa mdau mkubwa kwa kuhakikisha Haki Jinai na Utawala Bora vinapewa nafasi kubwa hapa nchini, na hata kusukuma utoaji wa fedha za kujengwa Ofisi za Mashtaka na kusogeza huduma kwa wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Utawala,Katiba na Sheria, amesema wamefurahishwa sana na ujenzi wa Ofisi za Mashtaka na kusogeza karibu huduma kwa wananchi na kwamba Muhimili huo ni muhimu sana katika kuimarisha Amani ya Nnchi, na kwamba Kamati hiyo itakuwa ikichangiza Bajeti zao kupita na kujengwa Ofisi nyingi.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Zamda Shabani, ambao ndiyo walitoa ardhi na kujengwa Ofisi hiyo ya Taifa ya Mashataka Shinyanga, amewasisitiza Mawakili kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwamba wawe na ufanisi katika utendaji wao kazi katika kuwahudumia wananchi na kupata haki zao.

Naye Mshauri Mwelekezi wa ujenzi wa Ofisi hiyo ya Taifa ya Mashtaka Shinyanga Israel Masawe, akisoma taarifa ya Ujenzi amesema ulianza Oktoba 5, 2022, na umekamilika Marchi mwaka huu na kufunguliwa leo na gharama zake ni Sh.bilioni 2.1.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dk.Khatibu Kazungu akizungumza kwenye hafla hiyo ya ufunguzi wa Jengo jipya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Shinyanga.
Mkurugenzi Mkuu Mashtaka (DPP)Sylvester Mwakitalu akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Joseph Mkude ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Utawala,Katiba na Sheria,kwenye hafla hiyo.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwakilishi wa Wakili Mkuu wa Serikali James Kibamba akizungumza kwenye hafla hiyo.
Viongozi wakiendelea kuzungumza kwenye hafla hiyo.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Zamda Shabani akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mshauri Mwelekezi wa ujenzi wa Ofisi hiyo ya Taifa ya Mashtaka Shinyanga Israel Masawe akisoma taarifa ya ujenzi.
Hafla ya ufunguzi Jengo jipya la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Shinyanga ikiendelea.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dk.Khatibu Kazungu akikata utepe kufungua Jengo jipya la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Shinyanga.
Ufunguzi ukiendelea.
Muonekano wa Jengo Jipya ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Shinyanga.
Picha za pamoja zikipigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.

Post a Comment

0 Comments