RC MACHA ASIMULIA VIJANA WALIVYO ZI BETIA FEDHA ZA MKOPO HALMASHAURI ASILIMIA 10,ASISITIZA WANANCHI SHINYANGA WAFANYE KAZI KAMA ALIVYOELEKEZA RAIS SAMIA

RC MACHA ASIMULIA VIJANA WALIVYO ZI BETIA FEDHA ZA MKOPO HALMASHAURI ASILIMIA 10,ASISITIZA WANANCHI SHINYANGA WAFANYEKAZI KAMA ALIVYOELEKEZA RAIS SAMIA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa mpya wa Shinyanga Anamringi Macha, amewasihi viongozi kutoa elimu kwa wananchi wa Mkoa huo, kwamba wafanye kazi na kujipatia Maendeleo kama maelekezo yalivyotolewa na Rais Samia wakati wakiwaapisha viongozi mbalimbali hivi karibuni ambao aliwateuwa.
Amebainisha hayo leo kwenye hafla ya kukabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.

Amesema Moja ya Maelekezo ambayo ameyatoa Rais Samia katika Mkoa wa Shinyanga ni pamoja na kuwasisitiza wananchi wafanye kazi, na kuacha tabia ya kushinda vijiweni wakicheza Bao pamoja na Vijana kukesha kwenye Michezo ya Kamari  waki beti.
“Ukitaka kujua Mkoa huu wa Shinyanga ni kweli watu hawapendi kufanya kazi, kuna siku moja Kahama vijana walipewa pesa ya Mkopo zile asilimia 10 za Halmashauri, vijana wale zile pesa waligawana na kwenda kuzibetia na wakishinda wanachanga na kurejesha marejesho mwisho wa siku waliliwa na pesa zikapotelea huko,”amesema Macha.

“Baada ya kusitisha utoaji wa pesa cash za hii Mikopo, bali tutoe vitendea kazi ikiwamo kugawa Mashamba na Mbegu hatukuwaona kijana hata Mmoja, ndiyo ujue watu hawapendi kufanya kazi, lakini akina Mama kwenye Mikopo hii walikuwa wakiitendea haki za kujikwamua kiuchumi kuliko vijana na hawa ndiyo sababu Mikopo ilisitishwa,”ameongeza Macha.
Aidha, Macha amewakumbusha Watumishiwa Serikali Maagizo ambayo alitoa Rais kwamba wakasikilize kero za Wananchi, na kuagiza kwamba Mofisa Ardhi katika Halmashuri zote za Mkuoa huo kwamba wajipange kwenda Site katika maeneo ambayo yanalalamikiwa na siyo kusikiliza Migogoro hiyo Maofisini.

“Maofisa Ardhi wa Halmashauri Mjipange tutasikiliza Migogoro ya Ardhi kwenye eneo husika ambalo linalozozaniwa, na siyo Migogoro kusikilizwa Maofisini,tena tunapaswa tuwe na Mahema ya kufunga Ofisi za muda na kutatua Migogoro huko huko Site,”amesema Macha.
Amewataka pia Watumishi wa Serikali wasijihusishe na masuala ya siasa na kuanza kutafuta nani wa kuwaongoza hasa kwenye kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu mwakani, kwamba jambo hilo waviachie vyama vya siasa, huku akiwasihi kufanya kazi bila mafarakano na chuki.

Katika hatua nyingine amewataka Watumishi wa Serikali,kutoa ushirikiano kwa Waandishi wa habari pale wanapokuwa wakihitaji taarifa mbalimbali kwa maslahi mapana ya jamii, na kwamba milango yake yeye ipo wazi kwa Mwaandishi yoyote atakayehitaji taarifa.
Naye aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, ameshukuru Watumishi wa Serikali mkoani humo kwa kumpatia ushirikiano, huku akiwasihi pia wampatie ushirikiano Mkuu huyo wa Mkoa mpya ili kusukuma maendeleo ya Shinyanga.

Aidha, ametumia fursa hiyo kuwataka pia wananchi wa Mkoa wa Shinyanga hasa wanawake, kwamba wajikite kwenye Matumizi ya Nishati safi ya kupikia pamoja na kutunza Mazingira kwa kuunga Juhudi za Rais Samia kwa kutaka Mazingira yatunzwe.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha (kulia) akikabidhiwa Ofisi na Nyaraka mbalimbali za utendaji kazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Christina Mndeme ambaye ameteuliwa na Rais Samia kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya Ofisi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya Ofisi.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Christina Mndeme ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Ofisi kwa RC Macha na kuwaaga Wana Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Christina Mndeme ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Ofisi kwa RC Macha na kuwaaga Wana Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.


Hafla ikiendelea.


Watumishi wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakimpatia Zawadi aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi akimpatia Zawadi aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kulia) akimpokea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha katika hafla ya kukabidhiwa Rasmi Ofisi.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kulia) akimpokea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha katika hafla ya kukabidhiwa Rasmi Ofisi.


Picha ya pamoja ikipigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464