KAMATI YA BUNGE PAC IMETEMBELEA MRADI WA UBORESHAJI USALAMA WA MILIKI ARDHI "LTIP" MANISPAA YA SHINYANGA

KAMATI YA BUNGE PAC IMETEMBELEA MRADI WA UBORESHAJI USALAMA WA MILIKI ARDHI  'LTIP'MANISPAA YA SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imetembelea Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Miliki Ardhi (LTIP) Manispaa ya Shinyanga, na kuwataka wananchi wachangamkie fursa ya kupata Hati Miliki.
Ziara hiyo imefanyika leo Marchi 20,2024 kwa kuona shughuli ambazo zinafanyika za kutambua,kupanga,kupima na kumilikisha wananchi Ardhi kwa kuwapatia Hati Miliki.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge (PAC) Japhet Hasunga, amesema Kamati hiyo kazi yake ni kusimamia na kuona Fedha za Umma ambazo ziliidhinishwa na Bunge, namna zinavyofanya kazi na kuleta Tija kwa Wananchi na kuonekana thamani yake.
“Sera ya Bunge tunataka kila kipande cha Ardhi kipimwe na kupangiwa Matumizi ili tuweze kusonga Mbele,”amesema Hasunga.

Aidha, amewataka wananchi wasiishie tu kwenye upimaji na utambuzi, bali wahakikishe wawe na Hati Miliki, na kwamba wakiwa na Hati Miliki eneo hilo ndiyo linakuwa la kwao kihalali.
Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geofrey Pinda, amesema Mradi huo ni Mkakati wa kutatua Migogoro ya Ardhi na Mipaka, pamoja na kuweka vizuri Mipango bora ya Matumizi ya Ardhi.

Amesema kwa Migogoro yote ya Ardhi ambayo ilikuwepo hapo awali, Mradi huo ndiyo umekuja kuitatua pamoja na wananchi kupata Hati Miliki ya Maeneo yao.
Naye Afisa Mipango Miji Manispaa ya Shinyanga Emmanuel Mitinje, amesema kwa Manispaa ya Shinyanga wameanza kupima katika maeneo ambayo yalikuwa yamejengwa Kiholela ili kupanga Miji pamoja na kurasimisha wananchi wapate Hati Miliki.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge (PAC) Japhet Hasunga akizungumza kwenye ziara hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge (PAC) Japhet Hasunga akizungumza na wananchi wa Kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga na kuwataka wachangamkie mradi huo kupata Hati Miliki za maeneo yao.
Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geofrey Pinda, akiendelea utekelezaji wa Mradi huo katika Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geofrey Pinda akizungumza kwenye ziara hiyo ya Kamati ya Bunge PAC.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akizunguzam kwenye ziara hiyo ya Kamati ya Bunge PAC.
Wananchi wa Kata ya Ibdakuli Manispaa ya Shinyanga wakiendelea na zoezi la urasimishaji Makazi yao.
Kamati ya Bunge PAC wakiwa ziara Manispaa ya Shinyanga kuona utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Miliki Ardhi (LTIP).
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464