JUKWAA LA MAENDELEO YA USHIRIKA MKOA WA SHINYANGA LAFANA,VYAMA VYA USHIRIKA VIMEAGIZWA KUINGIA KWENYE MFUMO WA TEHAMA

JUKWAA LA MAENDELEO YA USHIRIKA MKOA WA SHINYANGA LAFANA, VYAMA VYA USHIRIKA VIMEAGIZWA KUINGIA KWENYE MFUMO WA TEHAMA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
JUKWAA la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Shinyanga limefanyika kwa mara nyingine tena, na kuhudhuriwa na wadau na Vyama Mbalimbali vya Ushirika, huku yakitolewa maelekezo kwamba Vyama vyote vya Ushirika viingie kwenye Mfumo wa TEHAMA.

Jukwaa hilo limefanyika leo Marchi 21,2024 katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi Shinyanga, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Juma Mokili Juma akimwakilisha Mrajisi wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dk. Benson Ndiyege.
Juma akizungumza kwenye ufunguzi wa Jukwaa hilo ambalo litafanyikwa kwa muda wa siku mbili,amesema Mrajisi huyo amemtuma kwamba Vyama vyote vya Ushirika bila kusita vinapaswa kuingia kwenye Mfumo wa TEHAMA, ambao utaunganisha Mfumo wa usimamizi na uendeshaji wa Vyama vya Ushirika ‘Move’.

Amesema kwamba Mrajisi wa vyama vya Ushirika akihitaji kupata taarifa ya Chama chochote cha Ushirika apata kupitia Mfumo huo wa ‘Move’ hivyo kila Chama kinaagizwa kuanzia sasa kiwe na nyenzo au vifaa vyovyote ambavyo vitatumika kwenye Mfumo wa TEHAMA ikiwamo Computer, Laptop na Vishikwambi.
Amesema Vyama vya Ushirika pia viendelee kuzingatia, kutekeleza Kanuni, Sheria na Miongozo 15 ya Vyama vya Ushirika, na kwamba miongozo hiyo bado haijatendewa haki, huku akisisitiza kuandikisha wanachama kwenye Mfumo wa ‘Move’ na watakaofanya vizuri watapewa zawadi.

“Uandikishaji mfumo wa usimamizi na uendeshaji wa vyama vya Ushirika ‘Move’Mkoa wa Shinyanga umeunganisha Wanachama na Wakulima 72,000 na kushika nafasi ya Tatu katika Mikoa 26,”amesema Juma.
Maagizo mengine amesema ni kuendelea kuchangia Mtaji wa kuwezesha Benki ya Taifa ya Ushirika, na kwamba Kati ya Sh,milioni 153 ya fedha za Mtaji wa Benki hiyo zinatoka Mkoa wa Shinyanga.

Amesema pia Vyama vya Ushirika vinapaswa kutambua Mali zote za Ushirika na kuzirasimisha na kwamba Vyama vingi vinapata Hati zenye Mashaka kutokana na kutotambua Mali za Chama,huku akiupongeza Mkoa wa Shinyanga kwa kupata Hati Safi 46 kutoka 7.
“Navipongeza pia Vyama vya Ushirika Shinyanga kwa kulipa Malipo ya Pili ya Wakulima, na sisi Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania tuna ahidi kuendelea kushirikiana na Vyama vya Ushirika pamoja na kurudisha Mali za Vyama vya Ushirika, sababu tuna taarifa kwamba kuna watu walionyang’anywa mali za Ushirika wamekata Rufaa Mahakamani,”amesema Juma.

Mrajisi Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Hilda Boniphace, akielezea hali halisi ya Ushirika Mkoa wa Shinyanga, amesema Mkoa huo una Vyama vya Ushirika 273 ambavyo vyote hivyo wamefanikiwa kuvisajili kwenye Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika ‘Move’.
“Tunaipongeza Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa kutuletea Mfumo huu wa “Move’ ambao umeturahisishia kazi kwa maana ya usimamizi ambao ilikuwa Mtu hadi alete Mkataba wake lazima muonane uso kwa uso kwa hiyo unapunguza Urasmu na uonevu, sasa hivi Mkataba, Makisio na nyaraka zote vinapita kwenye mfumo wa wa Vyama vya Ushirika“Move” kuja kwa Mrajisi kupata idhini,”amesema Hilda.

“Mwaka 2023 tulikuwa tumesajili Wakulima na Wanachama 15,400 katika Vyama vyote 273 katika Mfumo wa “Move’ na mpaka sasa hadi Marchi tumesajili Wakulima na Wanachama 72,000,”ameongeza Hilda.
Aidha, amesema katika Mkoa wa Shinyanga wametekeleza vipaumbele 7 ambavyo nimaagizo ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika katika kuhakikisha vinaweka Ushirika katika hali ya kisasa zaidi, na kwamba kipaumbele namba moja ni uwekezaji katika Mfumo wa Kidigital.

Kipaumbele kingine ni kuharakisha mchakato wa uanzishaji wa Benki ya Taifa ya Ushirika kwa kununua Hisa na kuwekeza kwenye benki hiyo, kuhamasisha Mfumo wa Ushirikia kujiendesha Kibiashara, kuboresha Sera na Sheria ya Vyama Vya Ushirika, kuhamasisha Ushirika katika Sekta mbalimbali yakiwamo Makundi Maalumu.
Ametaja Kipaumbele namba Sita ambacho wamekitekeleza ni kuimarisha uwekezaji wa Mali za Ushirika na kuzithaminisha na kwamba Mali za SHIRECU zipo 82 KACU 62 na zote zimesha rasimishwa na kipaumbele cha Saba ni kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuendesha na kusimamia Sekta ya Ushirika Nchini.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Shinyanga (SHIRECU)Josephat Limbe,amesema Mkakati wa Chama hicho katika kumuinua Mkulima kiuchumi kwamba wamejipanga kukarabati Kiwanda cha kukamua Mafuta Kilichopo Mhunze pamoja na Gineri ya Mhunze ya kuchakata Zao la Pamba.
Naye Mjumbe wa Bodi wa Chama Kikuu Cha Ushirika Kahama (KACU) Emmanuel Nyambi akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa KACU Tano Nsambi, amesema Chama hicho kina Wanachama 138 wa Zao la Pamba 36 na Tumbaku 58, na Vyama vya Mazao Mchanganyiko 44.

Amesema Chama hicho kimepata mafanikio mengi ikiwamo kuongeza uzalishaji wa Zao la Tumbaku, kuongeza Bei kutoka Dola 1.6 hadi Dola 2, kuongeza wanunuzi wa Tumbaku, pamoja na kulipa Malipo ya Pili kwa Wakulima wa Zao la Pamba.
Jukwaa hilo la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Shinyanga litahitimishwa kesho.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Juma Mokili Juma akizungumza kwenye Jukwaa hilo.
Mrajisi Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Hilda Boniphace akizungumza kwenye Jukwaa hilo.
Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Simon Ntemi akizungumza.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Shinyanga (SHIRECU)Josephat Limbe akizungumza kwenye Jukwaa hilo.
Mjumbe wa Bodi wa Chama Kikuu Cha Ushirika Kahama (KACU) Emmanuel Nyambi akizungumza kwenye Jukwaa hilo.
Wajumbe wakiwa kwenye Jukwaa hilo.
Wajumbe wakiwa kwenye Jukwaa hilo.
Wajumbe wakiwa kwenye Jukwaa hilo.
Wajumbe wakiwa kwenye Jukwaa hilo.
Wajumbe wakiwa kwenye Jukwaa hilo.
Wajumbe wakiwa kwenye Jukwaa hilo.
Vyeti vya pongezi vikitolewa kwa waliochangia Hisa kwenye Benki ya Taifa ya Ushirika (KSBL).
Vyeti vya pongezi vikiendelea kutolewa.
Vyeti vya pongezi vikiendelea kutolewa.
Vyeti vya pongezi vikiendelea kutolewa.
Vyeti vya pongezi vikiendelea kutolewa.
Vyeti vya pongezi vikiendelea kutolewa.
Awali Maandamano yakiendelea kwenda kwenye Jukwaa hilo la Maendeleo ya Ushirika.
Maandamano yakiendelea ya Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika.
Maandamano yakiendelea ya Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika.
Maandamano yakiendelea ya Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika.
Maandamano yakiendelea ya Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika.
Maandamano yakiendelea ya Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464