KONGAMANO LA WANAWAKE NA WASICHANA 'CHANUO SUMMIT' LAFANA

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Wanawake na Wasichana wameshauriwa kuondoa hofu wanapotaka kuanzisha biashara ili kujinyanyua kiuchumi kupitia fursa mbalimbali ikiwemo kilimo, uvuvi na madini.

Ushauri huo umetolewa na wataalam mbalimbali leo Machi 30, 2024 katika kongamano la Wanawake na Wasichana Kanda ya Ziwa linaloitwa CHANUO SUMMIT lenye kauli mbiu isemayo JISUKE UISUKE DUNIA lililoratibiwa na Kampuni ya Jambo Group.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara, Kilimo na Viwanda Mkoa wa Shinyanga (TCCIA) Jonathan Manyama amesema hofu ndiyo inayokatisha tamaa Wanawake na Wasichana wanapotaka kuanzisha biashara hivyo kuwashauri wasiangalie nyuma.

“Kongamano hili limekuwa zuri kwa kuwaleta pamoja wafanyabiashara wazoefu na wale wanaotaka kuanza wajifunze zaidi hivyo Jambo FM wamefanya kitu kikubwa sana”,amesema Manyama.

Naye Meneja wa Jambo Media, Nickson George amesema uanzishwaji wa kongamano hilo na neno Chanuo umebeba dhamira kuu kwa wanawake na wasichana kutengua maisha yao kwa kupitia fursa, hivyo kwa kanda ya Ziwa wanahitaji kupata elimu zaidi ikiwa leo wamekuja na mada tatu muhimu za kuwajenga ambazo ni Kilimo, Uvuvi na Madini.

Amesema kongamono hilo ni mwendelezo wa makongamano mengine ya kimataifa kuwakutanisha wafanyabiashara Wanawake na Wasichana walio wazoefu na chipukizi kwa kukutanisha nchi za Afrika mashariki ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda na Ethiopia.

“Kanda ya ziwa katika utafiti uliofanyika ina watu takribani Milioni 17 ambao kila siku wana mahitaji, tumeona kuchukua fursa ya kuwafundisha Wanawake na Wasichana wanaopitia changamoto nyingi za kuweza kujikomboa kiuchumi na kutumia fursa zilizopo”,amesema George

Naye Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP  Janeth Magomi amesema jeshi hilo litaendelea kuimarisha usalama kwa Wanawake na Wasichana dhidi ya vitendo vya ukatili kupitia dawati la jinsia

Hellen Samson mkulima wa zao la mkonge kutoka wilayani Kishapu amesema ameweza kunufaika kupita zao hilo na soko lipo ambapo  anawashauri wanawake wenzake na wasichana kujifunza mbinu mbalimbali za kilimo na biashara ili wajinyanyue kimaisha kwani zao hilo halina changamoto kubwa kama wanavyofikiria.

Bwana shamba kutoka kampuni ya Burton Tanzania inayojishughulisha na kilimo cha nyanya Bernad Musiba amesema zao hilo kwa kanda ya ziwa linapata soko kubwa changamoto inayowafanya wafanyabiashara waliogope namna wanavyopata changamoto na kuanza bila kufanya utafikiti wa kina. 

Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria kongamano hilo wamesema kongamano hilo limewawezesha kubadilishana mawazo na kujifunza kwa kuondoa hofu na kila mwaka liwepo kongamano hilo wajifunze zaidi.
Meneja mkuu Jambo Media, Nickson George akielezea lengo la kongamano la Wanawake na Wasichana Kanda ya Ziwa linaloitwa CHANUO SUMMIT
Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara, Kilimo na Viwanda Mkoa wa Shinyanga (TCCIA) ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa shirika la Thubutu Africa Bwana Jonathan Manyama akizungumzia uwekezaji katika biashara na fursa zilizopo.
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP  Janeth Magomi akizungumza kwenye kongamano hilo.

Wanawake na Wasichana wakifuatilia kongamano hilo la kanda ya ziwa ambalo limeanza rasmi Mwaka huu 2024
Wanawake na Wasichana wakifuatilia kongamano hilo la kanda ya ziwa ambalo limeanza rasmi Mwaka huu 2024
Wanawake na Wasichana wakifuatilia kongamano hilo la kanda ya ziwa ambalo limeanza rasmi Mwaka huu 2024
Wanawake na Wasichana wakifuatilia kongamano hilo la kanda ya ziwa ambalo limeanza rasmi Mwaka huu 2024
Wanawake na Wasichana wakifuatilia kongamano hilo la kanda ya ziwa ambalo limeanza rasmi Mwaka huu 2024
Wanawake na Wasichana wakifuatilia kongamano hilo la kanda ya ziwa ambalo limeanza rasmi Mwaka huu 2024
Wanawake na Wasichana wakifuatilia kongamano hilo la kanda ya ziwa ambalo limeanza rasmi Mwaka huu 2024
Wanawake na Wasichana wakifuatilia kongamano hilo la kanda ya ziwa ambalo limeanza rasmi Mwaka huu 2024
 Bwana Shamba kutoka Burton Tanzania Bw.Benard Musiba  (kulia) akizungumzia fursa za uwekezaji katika Kilimo cha zao la nyanya kwa hadhara iliyohudhuria Chanuo Summit ambapo ameelezea changamoto za zao hilo pamoja na mbinu na njia za kukabiliana nazo ili kuhakikisha mkulima anapata faida kupitia zao hilo, upande wa kushoto ni mmoja wa watangazaji kutoka Jambo FM Ibrahim Mwakyoma.
 
Wanawake na Wasichana wakifuatilia kongamano hilo la Kanda ya Ziwa ambalo limeanza rasmi Mwaka huu 2024
Jackline Charls kutoka Jambo Fm akizungumza kwenye hafla hiyo.
Jackiline Charles kutoka Jambo FM akifanya mahojiano na mkulima wa zao la Katani kutoka Wilaya ya Kishapu Bi. Helena Samson (kulia).

Mfanyabiashara wa Samaki Sokoni Bwana John Maleke upande wa kulia akielezea fursa mbalimbali.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464