Askofu Sangu: pokea rushwa lakini usimpigie Kura
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
ASKOFU wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu,amewataka wananchi kwamba wasiwapigie Kura viongozi wanaotaka Madaraka kwa Rushwa.
Mwaka huu 2024 kuna uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa na Mwakani 2025 kuna uchaguzi Mkuu wa Madiwani,Wabunge na Rais.
Askofu Sangu amebainisha hayo leo Machi 31, 2024 kwenye Ibada ya Pasaka katika Kanisa Katoliki Parokia ya Ngokolo.
Amesema Mgombea akitoa Rushwa pokea lakini usimpigie Kura, na kwamba wananchi wanapaswa kuwa macho sana na viongozi wanaotaka Madaraka kwa Rushwa sababu ni wabinafsi na siyo wazalendo.
"Akikupa Rushwa pokea si amekupa, lakini kwenye sanduka hakuna kumpigia kura, kuweni Makini sana na watu wanaotafuta madaraka kwa Rushwa siyo Wazalendo, daima ni wabinafsi tuwe nao macho," amesema Askofu Sangu.
Amewataka pia Wananchi wale wenye uwezo na sifa ya kuwa viongozi, wa chukue fomu wagombee kwenye uchaguzi,wakiwamo Wanawake na vijana.
"Akina Mama chukue fomu Mgombea uongozi, Rais wetu ni Mwanamke, Spika wa Bunge Mwanamke na mnauwezo mkubwa wa kuongoza sababu mpo watulivu, pia na vijana tujitokezeeni kugombea kwenye hizi chaguzi," amesema Askofu Sangu.
Aidha, amewataka pia Watanzania kuombea Amani uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka huu,kwamba upite salama pamoja na kufanyika kwa haki na siyo kuvuruga Amani ya nchi.