Header Ads Widget

KATAMBI AUNGURUMA KITANGILI,FEDHA ZA JIMBO ZAMWAGWA KILA KATA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO


KATAMBI AUNGURUMA KITANGILI,FEDHA ZA JIMBO ZAMWAGWA KILA KATA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MBUNGE Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,amesema ahadi ambazo aliwahidi wananchi kipindi cha uchaguzi Mkuu 2020 nyingi amezitekeleza na kuwaletea maendeleo wananchi wa Shinyanga,huku akitoa fedha za jimbo Sh.milioni 61.6 ambazo zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kila Kata.

Amebainisha hayo leo Marchi 13,2024 wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Kitangili kwenye Mkutano wa hadhara.
Katambi ambaye pia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, amesema kutokana na machungu aliyonayo kwa wananchi wa Shinyanga, amekuwa akitafuta fedha ili kuteleza Miradi mingi ya Maendeleo,na kwamba ahadi ambazo alikuwa ameahidi nyingi ametekeleza.

"Ahadi ambazo niliwahidi wananchi kipindi cha uchanguzi nyingi nimetekeleza na nina Mshukuru Rais Samia kwa kuniunga mkono na leo kero nyingi zimetatuliwa ikiwamo miundombinu ya Barabara ambayo ilikuwa korofi na Madaraja," amesema Katambi.
"Mimi namapenzi mema na wananchi wa Shinyanga, na nitaendelea kuwaletea maendeleo siyo mtu wa starehe, Mfano Fedha za Jimbo za Mwaka Jana Sh.milioni 61.6 nimezigawa zote kwenye Kata ili zikatekeleze Miradi ya Maendeleo, ninge kuwa na tamaa ya fedha si ningekula," ameongeza Katambi.

Amesema kwa upande wa fedha ambazo amezitoa katika Michango mbalimbali kwa Chama, Taasisi za dini na Jamii, kipindi cha kuanzia Januari hadi Marchi mwaka huu ni Sh.milioni 41.7.
Aidha,Katambi ameeleza kuchukizwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiwapiga Majungu viongozi na kuwafanya fitina za ajabu, bali waache tabia hiyo ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Amesema kazi iliyobaki kwa wananchi ni kuwaunga mkono viongozi wanaotakana na CCM pamoja na kuwapigia Kura nyingi za ushindi akiwamo Rais Samia ili waendelee kuwaletea maendeleo.
Diwani wa Kitangili Mariamu Nyangaka,ameshukuru Katambi pamoja na Rais Samia kwa kumuunga Mkono na kufanikisha ujenzi wa Miundombinu ya Barabara na Madaraja ambayo yalikuwa kero kubwa za wananchi,huku akiahidi kuendelea kumalizia kero zilizobaki.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe, ametoa wito kwa wananchi kwamba kutokana na kasi kubwa ya Maendeleo ambayo wameletewa wawaunge Mkono viongozi wote wa CCM na kuwapigia Kura kwa wingi.
Katika ziara hiyo ya Katambi ameambatana pia na Madiwani wote wa Manispaa ya Shinyanga na kuelezea utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa wananchi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu,akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe akizungumza kwenye Mkutano huo.
Diwani wa Kitangili Mariamu Nyangaka akizungumza kwenye Mkutano huo.
Viongozi Meza Kuu wakiwa kwenye Mkutano huo.
Viongozi wakiwa kwenye Mkutano huo.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano huo.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wananchi wa Kitangili wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wananchi wa Kitangili wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wananchi wa Kitangili wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wananchi wa Kitangili wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wananchi wa Kitangili wakiwa kwenye Mkutano huo.

Post a Comment

0 Comments