Header Ads Widget

SAVE THE CHILDREN,RAFIKI SDO WAMETOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA SERIKALI USHIRIKISHAJI WATOTO KATIKA MIPANGO YA MAENDELEO


SAVE THE CHILDREN,RAFIKI SDO WAMETOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA SERIKALI USHIRIKISHAJI WATOTO KATIKA MIPANGO YA MAENDELEO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
SHIRIKA la Save the Children pamoja na Rafiki SDO,wametoa mafunzo kwa Watumishi wa Serikali halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Viongozi mbalimbali ngazi ya Kata juu ya ushirikishaji watoto katika upangaji wa Mipango ya Maendeleo na kuzingatia vipaumbele vyao.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza kutolewa leo Marchi 13,2024, yakihusisha Watumishi wa Halmashauri kutoka Idara ambazo zinahusika moja kwa moja na masuala ya watoto, na viongozi ngazi ya Kata na Madiwani kwa ufadhili wa Shirika la SIDA.
Afisa Miradi kutoka Shirika la Save the Children Victor Mkiza, akizungumza kwenye Mafunzo hayo, amesema wamewajengea uelewa Watumishi wa Halmashauri, na Viongozi wengine ngazi ya Kata juu ya kushirikisha watoto kwenye Mipango mbalimbali ya Maendeleo na kutoa mapendekezo yao na kupewa kipaumbele.

"Mafunzo haya kwa viongozi hawa ni kuzingatia ushirikishaji watoto kwenye Mipango ya kimaendeleo kuanzia ngazi ya Kata hadi Halmashauri,ili watoe mapendekezo yao na Serikali iwajibike kutekeleza vipaumbele vyao," amesema Mkiza.
Naye Meneja Mradi wa (MKUA) kutoka Shirika la Rafiki SDO Maria Maduhu,amewaomba Watumishi wa Serikali kwamba vipaumbele ambavyo watukuwa wakivitoa watoto kwenye vikao hivyo vya Mipango ya Maendeleo zifanyiwe kazi na kutatua Changamoto ambazo zinawakabili na kutimiza ndoto zao.

Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Shinyanga Elizabeth Mweyo, amewapongeza wadau hao kwa kuendelea kufanya kazi ya utetezi wa haki za watoto, huku akiahidi kwamba Serikali itaendelea kushirikiana nao.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Afisa Miradi kutoka Shirika la Save the Children Victor Mkiza akitoa mafunzo hayo.
Afisa Miradi kutoka Shirika la Save the Children Victor Mkiza akiendelea kutoa mafunzo.
Afisa Miradi kutoka Shirika la Save the Children Victor Mkiza akiendelea kutoa mafunzo.
Meneja Mradi wa MKUA kutoka Shirika la Rafiki SDO Maria Maduhu, akizungumza kwenye Mafunzo hayo.
Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Shinyanga Elizabeth Mweyo akizungumza kwenye Mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye Mafunzo.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea katika kazi ya vikundi.
Mafunzo yakiendelea katika kazi ya vikundi.
Mafunzo yakiendelea katika kazi ya vikundi.
Picha ya pamoja ikipigwa.

Post a Comment

0 Comments