WAGANGA WANAOPIGA RAMLI CHONGANISHI KUFICHULIWA
MUUNGANO wa Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala (TATDM)Mkoa wa Shinyanga, umeahidi kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Jeshi la Polisi, pamoja na kuwafichua Waganga ambao siyo waadilifu na taaluma yao wakiwamo wanaopiga Ramli Chonganishi.
Hayo yamebainishwa jana na Mwenyekiti wa Muungano wa Umoja wa Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala mkoani Shinyanga David Simlembe kwenye kikao chao, kilichofanyika Mazingira ‘Center’ Manispaa ya Shinyanga.
Amesema Muungano wao umeweka mikakati kwa Waganga kufanya kazi zao kwa kufuata Sheria,Miiko na Taaluma yao, na kwamba kwa wale ambao watakwenda kinyume watawafichua na kisha kuchukuliwa hatua wakiwamo wanaopiga Ramli Chonganishi na hata kusababisha mauaji ya watu wasio na hatia.
“Sisi tutafanya kazi kwa ushirikiano kabisa na Jeshi la Polisi, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, ili tufanye kazi zetu za Kuagua kwa kutii sheria za nchi na kuzingatia Miiko na Taaluma yetu, na tutawafichua wale ambao watakuwa siyo waadilifu na taaluma yao,”amesema Simlembe.
Naye Katibu Mwenezi wa Muungano wa Waganga hao mkoani Shinyanga Christopher Kubanda, amewasihi Waganga wote mkoani humo kwamba wajisajili kwenye Muungano wao pamoja na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, ili wapate kutambulika kisheria na siyo kufanya kazi kienyeji.
Nao baadhi ya Waganga hao akiwamo Yusuph Shedafa, amesema Waganga wote kujiunga kwenye Muungano wao ni jambo la muhimu, sababu watabainika Waganga ambao ni Matapeli waliojificha kwenye Taaluma hiyo.
Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, amesema Jeshi hilo litashirikiana na Muungano huo, huku wakiwasihi Waganga Matapeli na wanaopiga Ramli Chonganishi pamoja na wale ambao hawafuati taratibu za na sheria za nchi waache tabia kwani watachukuliwa hatua.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mwenyekiti wa Muungano wa Umoja wa Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala mkoani Shinyanga David Simlembe akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Muungano wa Umoja wa Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala mkoani Shinyanga David Simlembe akiendelea akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu Mwenezi wa Muungano wa Waganga Mkoa wa Shinyanga Christopher Kubanda akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu Mwenezi wa Muungano wa Waganga Mkoa wa Shinyanga Christopher Kubanda akizungumza kwenye kikao hicho.
Waganga wa Tiba Asili na Mbadala wakiwa kwenye kikao chao.
Waganga wa Tiba Asili na Mbadala wakiendelea na kikao.
Waganga wa Tiba Asili na Mbadala wakiendelea na kikao.
Waganga wa Tiba Asili na Mbadala wakiendelea na kikao.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464