HOSPITAL YA SEKOUTOURE NA UTEKELEZAJI WA PROGRAM JUMUISHI YA MALEZI, MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO.
Na Tonny Alphonce, Mwanza
Program jumushi ya taifa ya malezi,makuzi na maeldeleo ya wali ya mtoto mwenye umri kati yamiaka 0-8 ,inasisistiza juu ya maazingira rafiki na shawishi ya mtoto kujifunzia ili kuufanyaubongo wa mtoto uende sambamba na umri wake,huu ni umri unaoamua hatma ya mtoto baadaya kuvuka umri wa miaka nane huku tafiti na wataalam wakisema kesho ya mtu inaanzakujengwa kwenye umri kati ya miaka 0-8.
Jijini Mwanza kuna maktaba ya mfano,ni chumba maalumu cha watoto kucheza kikiwakimepambwa na vifaa mbalimbali vya kuchezea watoto huku kuta zake zikiwa zimepambwa na michoro ya herufi mbalimbali.
Chumba hiki ukiingia kwa mara ya kwanza unaweza kudhani upo shuleni katika darasa la kisasala wanafunzi wa madarasa ya awali kwa kuwa chumba kinaongea.
Maktaba hii ipo katika Hospitali ya Mkoa ya Mwanza (Sekou Toure)na inaelezwa kuwa kwaTanzania Maktaba za watoto zipo mbili tu nchi nzima mmoja ikipatikana Mwanza na nyingine Agha Khana jijini Dar es Salaam maktaba hii ya watoto imewekwa hospitalini?
Afisa Ustawi wa jamii mkoa wa Mwanza Faithmary Lukindo anasema vyumba hivi ni muhimukwa kuwa vinasaidia watoto kupata nafuu ya magonjwa haraka lakini pia watoto kupatauchangamshi na kuweza kuwasiliana na wenzao kupitia michezo inayofundishwa katikaMaktaba hizo.
Afisa Ustawi wa jamii mkoa wa Mwanza Faithmary Lukindo akizungumzia namnaMaktaba ya Watoto inavyofanyakazi Faithmary amesema waliamua kuanzisha maktaba hii hospitalini ili kuwasaidia watoto ambaowamelazwa waweze kupata nafasi ya kujifunza kupitia Maktaba ya Watoto ambayo kiuhalisia
inawasaidia pia kupunguza maumivu ya ugonjwa wanaopitia kwa kipindi hicho.“Mtoto anapoendelea kukua magonjwa ni sehemu katika ukuaji wake lakini hata anapokuwaameugua ukuaji hausimami hatua za ukuaji zinaendelea kama kawaida na ubongo unaendeleakukua kama kawaida kwa hiyo maktaba hii inamsaidia mtoto kupata fursa ya kujifunza paleanapopata nafuu kidogo wakati akiendelea na matibabu”.alisema Faithmary
Kwa upande wake Teddy John, Afisa ustawi katika hospitali ya Sekou toure kitengo cha ustawi wa jamii amesema maktaba hii wa watoto inawasaidia sana watoto wanaolazwa kwa muda mrefu kupata nafasi ya kujifunza huku wakiendelea na matibabu.
Teddy John afisa ustawi katika hospitali ya Sekou Toure kitengo cha ustawi wa jamii akizungumzia faida wanayopata watoto katika chumba cha Maktaba ya Watoto
Teddy amesema kuna watoto wanalazwa miezi miwili au zaidi hii husababisha mtoto kupitwa namasomo lakini kupitia maktaba hii inawasaidia watoto kuendelea kujifunza na atakapo ponaanaweza kuendelea na masomo yake bila tatizo lolote.
“Kabla hatujaanzisha maktaba hii ya watoto ilikuwa mtoto anashinda wodini muda wote nailikuwa ikisababisha watoto kukosa amani na kulia muda wote lakini baada ya kuanzishamaktaba hii ya watoto tumeona tofauti maana mtoto akiisha ingia kwenye chumba hikianabadilika anachangamka anaanza kucheza kwa kuwa kuna vitu vingi vya michezotumewawekea”.alisema Teddy
Pendo Jackobo kutoka idara ya watoto ambaye ndio msimamizi wa watoto hao amesemaamekuwa akienda kuwachukua watoto mara baada ya daktari kupita na kuwapatia matibabu.
Amesema katika maktaba hiyo wapo watoto wanaojifunza kusoma na kuandika na wapo watoto ambao wao hucheza kupitia michezo mbalimbali iliyopo katika chumba hicho.
“Kwa kweli watoto hufurahia sana wanapokuwa hapa maana kuna midori kuna magariwanaendesha kiasi kwamba watoto wengine wakiishaingia maktaba kucheza huwa hawatakikuondoka kutokana na michezo iliyopo kuwavutia”.alisema Pendo
Mmoja wa wazazi ambae amelazwa hospitalini hapo kwa zaidi ya mwezi mmoja AnnastaziaNgodoki amesema mara ya kwanza msimamizi wa Maktaba ya Watoto alipoenda kumchukuamtoto wake alikuwa na wasiwasi kuwa mtoto wake ataenda kusumbua lakini ilikuwa tofauti naalivyofikiria.
Mzazi akicheza na watoto katika Maktaba ya Watoto michezo mbalimbali
“Matroni alipokuja kumchukua mtoto mara baada ya kutibiwa na daktari nilitaka kumkatalialakini nikashangaa nusu saa nzima kimya mtoto hajarudishwa maana namjua mtoto wangu huwamara nyingi anapenda kuwa na mimi tu sasa nikaamua kwenda kumuona nilipoingia kwenyeMaktaba hiyo ya Watoto nilishangaa ilivyo nzuri na nilishangaa kumuona mtoto wanguamechangamka anacheza utadhani haumwi”.alisema Annastazia
Bila shaka katika tafiti zilizopangwa kufanyika ili kusaidia mchakato wa kutengeneza taarifa yautekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto(MMMAM) kwa kutambua ubunifu, mbinu zilizoleta matokeo chanya, vizuizi na viwezeshiutaigusa hospitali hii ya mkoa wa Mwanza (Sekou Toure) kwa ubunifu huu wa kuwa na Maktaba ya Watoto kwaajili ya watoto wanaotibiwa katika hospitali hiyo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464