MBUNGE OLE SENDEKA ASHAMBULIWA KWA RISASI
HABARI zilizotufikia hivi Punde ni kuwa mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amenusurika kuuwawa baada ya watu wasiojulikana kushambulia gari lake kwa risasi zaidi ya Nne.
Imeelezwa kuwa Mbunge huyo pamoja na dereva wake wote wamenusurika baada ya gari lao kushambuliwa kwa risasi wakati wakiwa jimboni humo kwa ziara za kibunge.
Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo katika eneo hilo wameeleza kwamba walisikia milio ya risasi ikishambulia gari hilo baadaye washambuliaji hao kutoweka kusikojulikana.
Hata hivyo hakuna taarifa za kuwepo kwa majeraha ama aliyepoteza maisha kwenye tukio hilo na Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Manyara ili kupata undani wa tukio hili zinaendelea.
Shinyanga Press Club blog tunaendelea kufuatilia taarifa hizi kwa na tutakuletea taarifa za kina kuhusu tukio hili endelea kuwa karibu nasi wakati Wote.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464