Mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food Products Salum Hamis akizungumza na Rais wa Chemba TCCIA Taifa ambaye alitembelea kiwanda hicho akiwa na viongozi wa Chemba wa Mkoa
Suzy Butondo, Shinyanga blog
Rais wa Chemba ya Biashara Viwanda na kilimo Tanzania (TCCIA) Vicent Bruno Minja amempongeza Mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food Products Salum Hamis kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika Mkoa wa Shinyanga.
Minja ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea kiwanda hicho na kuangalia shughuli za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa katika kiwanda hicho jana, akiwa ameambatana na wajumbe wa TCCIA mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili wawekezaji, ili aweze kuzifikisha ngazi husika ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.
Minja ameshangazwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Salum Hamis katika mkoa wa Shinyanga na kuahidi kutoa ushirikiano kwa uongozi wa kiwanda hicho kutatua changamoto zinazo changia kukwama kwa uzalishaji katika kiwanda hicho.
"Hongereni sana kwa kufanya uwekezaji mkubwa huu kwani sikuamini kama Shinyanga nitakuta viwanda vikubwa nna hii, hivyo nikupingeze sana mkurugenzi kwa kuweza kuipendezesha Shinyanga.
Kwa upande wake Mmiliki wa kiwanda cha Jambo Food Products Hamis, amemshukuru Rais wa TCCIA kwa kufanya ziara katika kiwanda hicho na kumuomba kuendelea kutatua kero zinazowakabili wafanya biashara hali itakayosaidia wafanya biashara na kukua kiuchumi.
"Nashukuru kwa kutembelea kiwanda changu, tunapitia changamoto nyingi kama ulivyokuta leo hatuna umeme umeme hivyo udhalishaji kwa leo umesimama, na wafanyakazi lazima walipwe malipo yao na sisi ni walipa kodi wakubwa lakini tunapitia changamoto hizi, amesema Hamis,
Rais wa Chemba Taifa Vicent Bruno Minja akizungumza kwenye kiwanda cha Jambo food baada ya kutembelea kiwanda hicho

Rais wa Chemba Vicent Bruno Minja akizungumza na Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Jonathan Manyama