Header Ads Widget

RAIS WA TCCIA AWASHAURI WAFANYABIASHARA MKOA WA SHINYANGA KUUNGANA ILI KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOPO



Suzy Butondo Shinyanga press Blog

Rais wa Chemba ya Biashara Viwanda na kilimo Tanzania TCCIA Vicent Bruno Minja amewataka wafanyabiashara wote wa mkoa wa Shinyanga kuungana ili kuwa na nguvu ya kuongea na mamlaka ya serika ili kutatua changamoto zao kwenye mamlaka husika.


Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na wafanyabiashara wanachama wa TCCIA na wasiokuwa wanachama wa Mkoa wa Shinyanga na kusikiliza changamoto mbalimbali za kibiashara, ambapo pia ameahidi kuchukua changamoto zote kuzifikisha ngazi husika ili ziweze kutatuliwa kwa wakati.


Minja amesema wafanyabiashara wengi nchini wamekuwa wakikutana na changamoto nyingi kutoka halmashauri TRA, hali ambayo inawafanya kushindwa kufanya kazi zao kwa uhuru, hivyo amewaomba ili waweze kutatuliwa changamoto zao waungane kwa pamoja waweze kuwa na nguvu moja, ili waweze kuifikishia serikali changamoto wanazokumbana nazo ili ziweze kutatuliwa.


"Nia yangu ni kusikiliza kero mbalimbali za wafanyabiashara ili tuweze kuzifanyia kazi na kuzipeleka kwenye mamlaka husika, kwani kuna changamoto kubwa sana hasa kwa wakulima, sheria zinatungwa lakini zinakinzana na wafanyabiashara, pia lengo kubwa ni kusikiliza wafanyabiashara nchi nzima ili ili tuweze kutengeneza kitabu chenye taarifa ya mikoa yote ya Tanzania"amesema Minja.


"Tunatakiwa kupromoti wawekezaji wa ndani kwenda mikoa mingine, kwani chemba ina uwezo wa kuwatangaza wawekezaji wa ndani, ndiyo wanaweza kukamata uchumi na uchumi ukatulia, hawa wa nje ni kuja kuendeleza tu, lakini wa ndani ndiyo wenye viwanda vikubwa hapa nchini, pia Taasisi yetu haipambani na serikali inakaa na serikali ili kuhakikisha changamoto za wafanyabiashara zinatatuliwa "ameongeza Minja.


Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhulia kwenye kikao cha mazungumzo na Rais wa Chemba akiwemo Jackton Koyi na Charles Machali kutoka sekta binafsi, wamesema wafanyabiashara wanapata changamoto kubwa kwenye utitiri wa kodi hasa kwenye eneo la ushuru wa huduma, hivyo wameiomba serikali iondoe kodi zote ili wafanyabiashara waweze kufanya biashara zao kwa uhuru.


Mfanyabiashara wa mazao mchanganyiko Hassan Hassan amesema anaomba lirudishwe soko hulia ili kila mtu auze mazao yake pale anapoona masirahi, kwani kwa sasa bei haijulikani,wanaambiwa wapeleke mazao yao katika vyama vya msingi AMCOS hivyo mkulima anatakaiwa kuuza siku ya mnada ambapo bei yake haijulikani.


"Tunaambiwa tupeleke AMCOS na mazao hayo yauzwe siku ya mnada, ambapo naweza nikajitolea kukusanya kidogo kwa shilingi 800lakini bei ya mnada inakuwa 600 hivyo napata hasara kubwa naomba utusaidie Rais wetu tunateseka sana sisi wafanyabiashara wa mazao,"amesema Hassan


Jackton Koyi ambaye ni mjumbe wa bodi ya Chemba amesema Wafanyabiashara wana kero nyingi sana wengine wangeongea kwa kulia hapa,hivyo wengi hawajazungumza hapa, lakini kwenye taarifa yetu tutaziandaa na tutakuletea, niwaombe wafanyabiashara muendelee kupambana msikate tamaa.


"Rais wetu hapa ametushauri wafanyabiashara tuungane tuwe na nguvu moja,hivyo niwaombe tuunganeni ili umoja wetu uweze kutusaidia tuwe na sauti kubwa tuweze kusikilizwa kwani tunaamini tutasikilizwa"amesema Koyi.


Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga Jonathan Manyama amesema changamoto kubwa iliyopo kwa wafanyabiashara ni kodi na VAT wafanyabiashara wengi wanapoenda kulipa wamekuwa wakikosa hiyo VAT na kwenda kukopa benki hali ambayo imekuwa ikiwakatisha tamaa wafanyabiashara wengi.


"Nia yetu ni kuishauri serikali iweze kuwasaidia wafanyabiashara wote ziondolewe kodi ndogo ndogo kwani wengi wamekuwa wakilia kwamba wanafanya biashara faida hawaioni kutokana na kodi kuwa nyingi hivyo nikuiomba serikali iondoe kodi ndogo ndogo ili waweze kufanya biashara zao maana wengine wanashindwa kuendelea kutokana na kuwa na kodi nyingi"amesema Manyama.
Rais wa Chemba ya Biashara Viwanda na kilimo Tanzania TCCIA Vicent Bruno Minja akizungumza na mwenyekiti wa TCCIA Jonathan Manyama katikati kulia ni Mjumbe wa Bodi Jackton Koyi
Mjumbe wa bodi ya Chemba Mkoa wa Shinyanga Jackton Koyi akizungumza kwenye kikao cha Rais wakati kizungumza na wafanyabiashara
Wajumbe wa kikao hicho wakiwa kwenye picha ya pamoja
Wajumbe wa kikao hicho wakiwa kwenye picha ya pamoja
Wajumbe wa kikao hicho wakiwa kwenye picha ya pamoja
Wajumbe wa kikao hicho wakiwa kwenye picha ya pamoja
Katibu wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga akizungumza
Mmoja wa wafanyabiashara akizungumza

Mmoja wa wafanyabiashara Wambura ambaye ni mkurugenzi wa Karena Hotel akizungumza
Mjumbe wa Mkutano huo akizungumza
Mjumbe wa Mkutano huo akizungumza
Mjumbe wa Mkutano huo akizungumza
Mjumbe wa Mkutano huo akizungumza
Wafanyabiashara wakimsikiliza Rais bada ya kutoa kero zao
Wafanyabiashara wakimsikiliza Rais bada ya kutoa kero zao
Dkt. Elyson Maeja akizungumza kwenye mkutano huo







Post a Comment

0 Comments