Rais wa
Chemba ya Biashara Viwanda na kilimo Tanzania TCCIA Vicent Bruno Minja akizungumza na mkurugenzi wa shule ya sekondari Kom Jackton Koyi
- Suzy Butondo Shinyanga press blog
Mkurugenzi wa Shule ya Kom Sekondari iliyoko katika mtaa wa Butengwa manispaa ya Shinyanga Jackton Koyi ameiomba serikali iwaondolee kodi ndogo ndogo ambazo zimekuwa zikitozwa na serikali hali ambayo imekuwa ikisababisha kukosa gharama za uendeshaji wa shule.
Hayo ameyasema leo Rais wa
Chemba ya Biashara Viwanda na kilimo Tanzania TCCIA Vicent Bruno Minja kutembelea katika shule hiyo, ambapo amesema shule za binafsi zinapitia changamoto nyingi.
Koyi amesema mbali na kuwa na changamoto za kodi 20 pia TRA wamekuwa wakitaka kulipa kodi ya shilingi milioni 300 kwa mwaka, hali ambayo imekuwa ikiwatisha na kusababisha mishituko ya moyo kutokana na kuandikiwa kodi kubwa inayopita kiwango cha kile wanachokipata, huku ushuru wa huduma (Service leavy) wakilipa milioni 100 au 80.
"Unakuta katika shule hii tuna wanafunzi 1000 wanatakiwa kula kila siku,wafanyakazi zaidi 100, na ukiangalia sasa hivi hali ya kiuchumi kwa wazazi imeshuka,angalau tulikuwa tunaiomba serikali itufutie kodi ndogo ndogo ili shule zetu ziweze kujiendesha,"amesema Koyi
"Labda tungeambiwa kwamba kila mwanafunzi atozwe kodi ya shilingi 10000 badala ya sisi kutudai, hali ya kipato kwa watu imedorola tusiposaidiwa na serikali hizi shule tutazifunga, angalau serikali ituangalie na sisi hata kutuletea Ruzuku kidogo kidogo hata ya vitabu, tunachangamoto kubwa,"ameongeza Koyi.
Kwa upande wake Rais wa Chemba Taifa Minja amewataka wafanyakazi hao wasikate tamaa waendelee kusonga mbele serikali ni sikivu italifanyia kazi, kwani inasikia kilio cha kila mtu na kila sekta, cha muhimu mnatakiwa kushirikiana na Chemba na sasa kuna baadhi ya kodi zimefutwa.
"Tunaomba muendelee kusaidia Chemba ya mkoa ili iendelee kufanya vizuri zaidi katika kuwasaidia wafanyabiashara, kweli tuna changamoto nyingi wafanyabiashara kila kona wanalia, na mimi natembelea mikoa mbalimbali nakutana nachangamoto nyingi hivyo naamini serikali yetu tukiipelekea haya itatusaidia,"amesema Rais Minja.
Rais wa
Chemba ya Biashara Viwanda na kilimo Tanzania TCCIA Vicent Bruno Minja akizungumza na mkurugenzi wa shule ya sekondari Kom Jackton Koyi
Mkrugenzi wa shule ya Kom Jackton Koyi akizungumza na Rais wa i
Chemba ya Biashara Viwanda na kilimo Tanzania TCCIA Vicent Bruno Minja
Viongozi wa TCCIA wakiwa na Rais wa Chemba baada ya kutembelea katika shule ya sekondari Kom kwa ajili ya kuchua changamoto mbalimbali