UMUHIMU WA WAZAZI NA WALIMU KUTUMIA ZANA ZA KUJIFUNZIA KUWAFUNDISHA WATOTO
Na Tonny
Alphonce, Mwanza
Zana za kujifunzia
na kufundishia huwakilisha vifaa vyote ambavyo mwalimu hutayarisha na kutumia
wakati wa mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji ili zimrahisishie ufundishaji
wake na kuwafanya wanafunzi waelewe somo kirahisi zaidi.
Mwalimu anapotumia zana mwanafunzi hupata faida kwa kujifunza zaidi kwa kuona ,kugusa, kuonja,kunusa na kusikia kwa kutumia njia hii mtoto hufurahia somo pia humpatia mtoto maarifa na ujuzi kwa njia ya mkato na ujuzi wa maarifa hayo huwa vigumu kusahaulika upesi.
Pamoja na
faida hizo kumekuwa na tatizo la wazazi kushiriki katika kutengeneza zana hizo za kujifunzia
watoto ambapo baadhi ya wazazi hukwepa wakidhani ni gharama kubwa kuandaa zana
hizi ambazo kiuhalisia hutengenezwa na malighafi zilizopo katika mazingira yao
yanayowazunguka.
Shirika la
Tanzania Eary Childhood Education and Care -TECEC kwa kushirikiana na walimu wa
madarasa ya awali katika shule ya msingi
ya Luchelele pamoja na wazazi wameunda
zana na vifaa vya kujifunzia na kuchezea kwa watoto wa darasa la awali
kwa kutumia vifaa vinavyopatikana katika mazingira ya shule.
(PICHA)
Walimu wa madarasa ya awali katika shule ya
msingi ya Luchelele, Wazazi na Wanafunzi wakishiriki kutengeneza zana na
vifaa vya kujifunzia na kuchezea watoto.
Mkurugenzi
wa TECEC Joel Elphas anasema wao kama shirika wanajua umuhimu watoto kujifunza na kucheza na kupitia Zana
mbalimbali za kujifunzia kutaweza kukuza ujuzi wao wa kijamii, kiakili, kimwili
na kihisia.
Joel amesema
kupitia vifaa hivyo vya ubunifu vinatoa uhakika kwa watoto kupata fursa ya
kujifunza kwa njia ya vitendo na kujifurahisha, wakati pia wakichunguza
mazingira yao ya karibu.
“Mwanzoni
ilikuwa ngumu kuwapata wazazi ili nao washiriki katika utengenezaji wa zana
hizi lakini baada ya kuwaelimisha tumepata ushirikiano mkubwa na tumefikia
lengo kama taasisi kutengeneza zana nyingi ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwa
vijana”.alisema Joel
Amesema
wanajivunia kuwa sehemu ya juhudi hizo za kipekee kwa kuwa zimewezesha
upatikanaji wa elimu bora na fursa za kujifunza kwa watoto na amewashukuru walimu wa madarasa ya awali, wazazi na walezi
kwa mchango wao mkubwa na ushirikiano wao katika kufanikisha mradi huo wa
kutengeneza zana za kujifunzia.
Joel
amewataka wazazi kujenga utamaduni wa kutengeneza zana za kujifunzia wao pamoja
watoto wao kwa kuwa malighafi zote zinapatikana katika mazingira waliyopo na
kama watahitaji msaada wa kiufundi wanaweza kuwasiliana na shirika la TECEC kwa
msaada zaidi.
Ester
Macha ambaye ni mtaalamu wa elimu ya
awali kutoka TECEC amesema kuwa katika kutekeleza zoezi hilo wazazi na wanafunzi walishirikishwa ili kutoa mawazo
yao na michango yao ya ubunifu na kwa pamoja wakafanikiwa kutengeneza zana za
kujifunza ambazo zilikuwa rahisi kwa watoto kuelewa na kufurahia ujifunzaji
shuleni.
“Tulibaini
kwamba vifaa kama vile chupa za plastiki, maboksi,Sponji na vitu vingine vya
kawaida vinaweza kutumiwa kutengeneza zana hizi za kuchezea na kujifunza zikiwa
zinahitaji ubunifu bila gharama kubwa kwa kuwa
rasilimali zote zipo kinachohitajika ni kutengeneza tu vifaa
hivyo”.alisema Ester
Mwalimu wa darasa la awali Zawadi
Kokutangilila amesema ni vema wazazi na walimu kupewa ujuzi wa namna ya kutengeneza zana za
kufundishia kwa watoto wa madarasa ya awali kwa sababu itasaidia mtoto kuelewa
kwa urahisi kwa kuwa shuleni atafundishwa kwa kutumia Zana na akirudi nyumbani
atafundishwa na mzazi kwa kutumia tena Zana zilizopo nyumbani.
Mwalimu
Martin amesema ndio maana wanasisitiza katika madarasa ya awali ni vema walimu
wakatumia Zana zaidi katika kufundishia ili watoto wapate uelewa zaidi wa kile
mwalimu alichokusudia kukifundisha.
“Mwanafunzi
wa darasa la awali tukumbuke anafundishwa vitu vidogo vidogo kama kushirikiana
na wenzake,kujifunza lugha na kufundishwa kwa njia ya picha hayo ndio malengo
ya elimu ya awali”.alisema Mwl Nkwabi
Akizungumzia
umuhimu wa utengenezaji wa Zana kwaajili ya kufundishia watoto,Mwl Nkwabi
amesema walimu wamekuwa wakipewa elimu ya namna ya utengenezaji wa Zana kwa
kushirikiana na mashirika yanayotekeleza afua za watoto.
Nao wazazi
Joel Mafuru na Agness Masanja ambao
wamewahi kupewa elimu ya utengenezaji wa Zana wamesema mwanzoni hakuwakujua
kama zana hizo ni muhimu katika ujifunzaji wa mtoto lakini wameshuhudia jinsi
watoto walivyochangamka na kupata furaha wanapojifunza kupitia zana hizo.
“Kwa sasa
ninao uwezo wa kutengeneza zana hizi na kuanzia na nimefanikiwa kumtengenezea
mwanangu Zana mbalimbali ambazo zinamsaidia katika safari yake hii ya masomo ya
darasa la awali”.alisema Mafuru
Kanuni za
vituo vya kulelea watoto wadogo mchana na watoto wachanga ya mwaka 2012
inahusisha mchakato wa uandaaji wa
kiongozi cha utengenezaji wa vifaa vya michezo na kujifunzia watoto chini ya
miaka 5.
Vilevile,
uelewa juu ya umuhimu wa ujifunzaji kupitia michezo haukupewa kipaumbele katika
ngazi zote za maamuzi, udhibiti ubora, watoa huduma, waelimishaji na jamii kwa
ujumla ikiwemo wazazi.
Ukosefu wa vifaa vya kuchezea watoto, vitabu, uelewa na ujuzi kuhusu malezi na wazazi kutokuchangamana na watoto mara kwa mara nayo imeripotiwa kama changamoto
Pia Program Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi
na Maeldeleo ya Awali ya Mtoto Mwenye umri kati ya miaka 0-8 ,inasisistiza juu
ya maazingira rafiki na shawishi ya mtoto kujifunzia ili kuufanya ubongo wa
mtoto uende sambamba na umri wake,huu ni umri unaoamua hatma ya mtoto baada ya
kuvuka umri wa miaka nane huku tafiti na wataalam wakisema kesho ya mtu inaanza
kujengwa kwenye umri kati ya miaka 0-8. ndio maana