Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia akizungumza wakati akifunga mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia (katikati) akikagua vihenge vilivyotengenezwa na vijana walioshiriki mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa 'Tanzania Initiative for Preventing Aflatoxin Contamination – TANIPAC)' ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jumla ya vijana 19 kutoka Halmashauri za Wilaya ya Buchosa (Mwanza), Itilima (Simiyu) , Nzega (Tabora) na Bukombe (Geita) wamehitimu mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa 'Tanzania Initiative for Preventing Aflatoxin Contamination – TANIPAC)' ulio chini ya Wizara ya Kilimo kwa lengo la kuimarisha usalama wa chakula kwa wananchi na afya ya jamii.
Mafunzo hayo yaliyofanyika kuanzia Machi 14,2024 yakitolewa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) yamefungwa leo Jumatano Machi 27, 2024 katika ukumbi wa SIDO Mkoa wa Shinyanga na Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa TANIPAC unaolenga kuiwezesha jamii kutumia njia sahihi na za kisasa za uhifadhi wa nafaka hususani mahindi kutokana na sumukuvu.
"Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Kilimo imeingia gharama kuhakikisha kuwa vijana wanapatiwa ujuzi wa kutengeneza vifaa vya kisasa na vinavyodumu kwa muda mrefu ili kutimiza adhima ya kupunguza sumukuvu ili kuimarisha usalama wa chakula kwa wananchi lakini pia kuhakikisha vijana wanapata ajira kwa kujiajiri na kuajiri wengine”,amesema Elia.
Amesema kupitia mafunzo hayo, washiriki wamejifunza mbinu mbalimbali za utengenezaji vihenge kwa vitendo, ujasiriamali, masoko, usimamizi wa fedha na urasimishaji biashara hivyo kuwataka wakayatumie kwa vitendo ili kujipatia ajira na kutimiza malengo ya serikali ya kutokomeza sumukuvu na wakawe mabalozi wa kukemea matumizi yasiyo sahihi ya utunzaji wa nafaka yanayopelekea sumukuvu.
Aidha amewataka vijana hao wakazingatie kutengeneza vifaa vyenye ubora, kutumia muda vizuri, wajifunze kuweka akiba na kutumia lugha nzuri kwa wateja wao na watumie huduma zinazotolewa SIDO.
Akisoma Risala ya wahitimu wa mafunzo hayo, George Stanley Joseph amesema wamejifunza kuhusu ujasiriamali, masoko na huduma kwa wateja, usimamizi wa fedha, urasimishaji wa biashara na utengenezaji wa vihenge kwa vitendo na kwamba elimu na mafunzo waliyopata yatawasaidia kuboresha utendaji kazi na kuzalisha bidhaa za vihenge (Silos) na nyinginezo kwa tija ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.
"Tunaushukuru uongozi wa SIDO na Wizara ya Kilimo kwa kutoa fursa ya mafunzo haya ambayo yametujengea uwezo wa kujiamini na kuamsha ari ndani yetu ya kujiajiri na kuachana na kasumba ya kusubiri ajira”,amesema Joseph.
Mwenyekiti wa darasa la mafunzo ya utengenezaji Vihenge, Emmanuel Ngasa Masaka (kushoto) akimwelezea Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia kuhusu vihenge vilivyotengenezwa na vijana walioshiriki mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa 'Tanzania Initiative for Preventing Aflatoxin Contamination – TANIPAC)' ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia (kulia) akizungumza wakati akikagua vihenge vilivyotengenezwa na vijana walioshiriki mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa 'Tanzania Initiative for Preventing Aflatoxin Contamination – TANIPAC)' ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia (katikati) akizungumza wakati akikagua vihenge vilivyotengenezwa na vijana walioshiriki mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa 'Tanzania Initiative for Preventing Aflatoxin Contamination – TANIPAC)' ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia (katikati) akipiga picha ya kumbukumbu na vijana walioshiriki mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia akizungumza wakati akifunga mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia akizungumza wakati akifunga mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia akizungumza wakati akifunga mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia akizungumza wakati akifunga mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia akizungumza wakati akifunga mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Washiriki wa mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo wakiwa ukumbini
Mwenyekiti wa darasa la mafunzo ya utengenezaji Vihenge, Emmanuel Ngasa Masaka akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Mhasibu wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, bi. Misuka Makwaya akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo
George Stanley Joseph akisoma risala ya wahitimu wa mafunzo
Mratibu wa Mafunzo SIDO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Manyama Lububi akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Hafla ya kufunga mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC) ikiendelea

Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia (kulia) akimkabidhi cheti cha uthibitisho wa kushiriki mafunzo mmoja wa washiriki wa mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC)

Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia (wa tatu kulia waliokaa) akipiga picha ya kumbukumbu na washiriki wa mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC).
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog