ASKOFU MABUSHI AIPONGEZA SERIKALI KWA JITIHADA KUBWA ZA KUBORESHA HALI YA MIUNDOMBINU YA USAFIRI

Askofu David Mabushi akihubiri neno la Mungu Kanisani kwake

Na Suzy Butondo,Shinyanga blog

Askofu wa kanisa la  International Evangelical Assemblies of God Tanzania (IEAGT),David Mabushi amesema serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya  jitihada kubwa za kuboresha hali ya miundo mbinu ya vyombo vya usafiri kwa ajili ya kuifungua nchi na kuimarisha mawasiliano kwa ajili ya ustawi wa sekta zote.

Hayo ameyasema hivi karibuni wakati akihubiri neno la Mungu kanisani hapo, ambapo alisema  Tanzania imekuwa ikifanya jitihada kubwa na imefanikiwa kufanya jaribio la kutoa treni ya umeme kutoka jiji la Dar esa laam hadi Dodoma ambayo ni hatua kubwa kwa sekta ya uchukuzi na mawasiliano.


" Ndugu zangu hii ni dalili njema ya nchi yetu kufunguka kila eneo, na italeta fursa nyingi  kwa kila sekta kwa mawasiliano, ni nguzo ya ukuaji, kwa hatuna hii ni budi kumshukuru Mungu kwa baraka hizi tunazoendelea kuziona"amesema Mabushi.

Askofu Mabushi amesema kukamilika kwa mradi huo ni habari njema kwa wananchi wengi wanaoona, ambapo utawapuguzia adha ya usafiri hasa wakati huu ambapo matumizi ya barabara yamekuwa na changamoto kubwa ikiwemo vizuizi vinavyosababoishwa na askari wa usalama barabarani.

Aidha Mabushi amesema mradi huo wa treni ya umeme ulitazamiwa pia kuwa habari njema kwa nchi jirani kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda, ambazo hutegemea bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusafirishia mizigo yake.

"Nimpongeze sana Rais wetu Samia Suluhu pamoja na jopo lake la uongozi kwa kazi nzuri anazozifanya, hivyo tuendelee kumuombea ili aweze kufanya maendeleo makubwa katika Taifa letu la Tanzania"amesema Mabushi.

Kwa upande wake Wilson Lubasha ambaye ni mshirika wa kanisa hilo amesema kanisa limekuwa likiombea viongozi wa Tanzsnia waendelee kutekeleza  mipango mizuri ya nchi, na Mungu amejibu,hivyo maendeleo hayo ni faida ya ukuaji wa nchi  katika sekta ya usafiri kama nchi zilizoendelea zaidi.

Estomini Mmasy ambaye ni mshirika wa kanisa hilo amesema sisi waumini tunajukumu la kuliombea Taifa pamoja na viongozi wote ili waweze kufanya mabadiliko makubwa katika Taifa  la Tanzania. 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464