KANISA LA TAG SHINYANGA LIMEADHIMISHA MIAKA 85 YA KUANZISHWA KWA KANISA HILO NCHINI TANZANIA

KANISA LA TAG SHINYANGA LIMEADHIMISHA MIAKA 85 YA KUANZISHWA KWA KANISA HILO NCHINI TANZANIA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
KANISA la Tanzania Assemblies Of God (TAG)Rehoboth Christian Centre lililopo Ngokolo maeneo ya Mwoleka Manispaa ya Shinyanga, limeadhimisha miaka 85 ya kuanzishwa kwa Kanisa hilo hapa nchini.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo April 1,2024 Kanisa hapo ambayo yalitanguliwa na Maandamano kwa kuzunguka baadhi ya Maeneo ya Manispaa ya Shinyanga, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.
Katibu wa Kanisa hilo Gilselda Kasili akisoma historia ya kuanzishwa kwa Kanisa la TAG Tanzania, amesema lilianzishwa mwaka 1939 na Mmisionari Paul Deer wakati huo Tanzania ikiitwa Tanganyika.

Amesema mwaka 1981 Kanisa hilo lilisajiriwa Rasmi chini ya Sheria ya Society Ordinance ya mwaka 1954, na kupewa namba ya usajiri S0/6246, na kwamba Kitaifa mpaka sasa wana jumla ya Makanisa 15,904 na Washiriki 1,903,741, Wachungaji 15,890, Wasimikwa 5,879, Wahubiri 1,748 na Watendakazi 8,263.
Amesema kwa Mkoa wa Shinyanga Kanisa hilo liliingia mwaka 1968 na mpaka sasa Kanisa lina miaka 56, Washiriki wakiwa 400 Wanaume 90, Wanawake 197 na Watoto 113, na kwamba wameweza kuzalisha Makanisa mengine 19.

“Kanisa letu la Rehoboth Christian Centre TAG hapa Shinyanga tuna Mikakati ya kufanya ujenzi wa Makanisa mpya Matatu, na Mpango huu tayari tumeanza ujenzi katika Kanisa letu lililopo Mwawaza pamoja na ununuzi wa Kiwanja Maganzo,”amesema Gilselda.
Aidha, amesema Kanisa hilo limekuwa likitoa huduma za Kiroho pamoja na Kijamii, kwa kushirikiana Taasisi isiyo ya Kiserikali Commpassion International na kuwahudumia watoto wanaoishi katika Mazingira Magumu, na kwamba hadi sasa wameshahudumia watoto 250, Kiroho, Kimwili na Kiakili.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo la TAG Shinyanga Christian Kubena, amesema kufanya Maadhimisho ni kufuata Maandiko Matakatifu ya Mungu ya Kukumbuka, na kuyaishi mambo mazuri ya watangulizi katika kuongoza Kondoo wa Bwana.

Mgeni Rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amelipongeza Kanisa hilo la TAG kwa kuadhimisha miaka 85 ya kuanzishwa kwake,huku akiwataka Waumini walishike neno la Mungu ili wawe salama, na wasikubali kutekwa na muovu Shetani na hasa kupitia Mitandao ya Kijamii.

Aidha, Katika Madhimisho hayo Meya amechangia pia kiasi cha fedha Sh.500,000 kwa ajili ya kufanikisha ununuzi wa vyombo vya Mfumo wa TEHAMA na Mziki Kanisa hapo, ili visaidie kutangaza Injili na watu waijue kweli na kumfuata Mungu.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho hayo ya miaka 85 ya Kanisa la TAG, inasema “Miaka Kumi na tatu ya Moto wa Uamsho, tunamtaka Bwana na Nguvu zake,”

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la TAG Rehoboth Christian Centre Ngokolo Shinyanga Christian Kubena akizungumza kwenye Maadhimisho hayo ya Miaka 85 ya TAG Tanzania.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la TAG Rehoboth Christian Centre Ngokolo Shinyanga Christian Kubena akiendelea kuzungumza kwenye Maadhimisho hayo ya Miaka 85 ya TAG Tanzania.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la TAG Rehoboth Christian Centre Ngokolo Shinyanga Christian Kubena akiendelea kuzungumza kwenye Maadhimisho hayo ya Miaka 85 ya TAG Tanzania.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye Maadhimisho ya Miaka 85 ya kuanzishwa kwa Kanisa la TAG Tanzania.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akiendelea kuzungumza kwenye Maadhimisho ya Miaka 85 ya kuanzishwa kwa Kanisa la TAG Tanzania.
Katibu wa Kanisa la TAG Rehoboth Christian Centre Ngokolo Shinyanga Gilselda Kasili akisoma Historia ya kuanzishwa kwa Kanisa la TAG Tanzania.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la TAG Shinyanga Christian Kubena (kulia) akiwa na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko kwenye Maadhimisho hayo.
Kamati ya Maandalizi ya kuadhimisha Miaka 85 ya kuanzishwa kwa Kanisa la TAG Tanzania ikijitambulisha.
Maadhimisho ya miaka 85 ya kuanzishwa kwa Kanisa la TAG Tanzania yakiendelea katika Kanisa la TAG Rehoboth Christian Centre Ngokolo Shinyanga.

Nyimbo za Sifa zikiimbwa kwenye Maadhimisho hayo.
Nyimbo za Sifa zikiendelea kuimbwa kwenye Maadhimisho hayo.
Nyimbo za Sifa zikiendelea kuimbwa kwenye Maadhimisho hayo.
Nyimbo zikiendelea kuimbwa kwenye Maadhimisho hayo.
Nyimbo zikiendelea kuimbwa kwenye Maadhimisho hayo.
Awali waumini wakiwa kwenye maandamano katika kuadhimisha miaka 85 ya kuanzishwa kwa Kanisa la TAG Tanzania.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiwasili Kanisani
Watoto wakipiga picha ya Pamoja.
Watoto wakiendelea kupiga picha ya pamoja.
Watoto wakiendelea kupiga picha ya pamoja.
Muonekano wa Kanisa la TAG Rehoboth Christian Centre lililopo Ngokolo maeneo ya Mwoleka Manispaa ya Shinyanga.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464