DC MTATIRO ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI OLD SHINYANGA,ATOA MAAGIZO KWA WATENDAJI WA SERIKALI

DC MTATIRO ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI OLD SHINYANGA,ATOA MAAGIZO KWA WATENDAJI WA SERIKALI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MKUU wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro,amesikiliza kero za wananchi wa Kata ya Oldshinyanga na kuzitatua,huku akiwataka Watendaji wa Serikali wawe wanatatua kero za wananchi kwa wakati.

Mtatiro amebainisha hayo leo April 2,2024 Kwenye Mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za Wananchi wa Kata hiyo, uliofanyika Viwanja vya Zahanati ya Oldshinyanga.
Amesema yupo Shinyanga kwa ajili ya kufanya kazi ya kumsaidia Rais Samia, katika kuwahudumia Wananchi na kutatua kero zao ambazo zinawakabili, na kuwataka Watendaji wa Serikali kwamba wakiletewa kero yoyote waitatue kwa wakati.

"Kazi yetu sisi ni kuhudumia Wananchi kumsaidia Rais Samia, na mimi sitakuwa Mkuu wa wilaya wa kukaa Ofisini,bali ni kiongozi wa Field na kuwafuata wananchi hukohuko kwenye maeneo yao na kuwapatia huduma," amesema Mtatiro.
"Kwenye eneo langu mimi la kazi nataka kila Jambo liwe limenyooka, ndiyo maana nafanya Mikutano ya hadhara ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua, na kama Mwananchi unashida usisubili Mikutano tumieni namba yangu kunipigia 0739-420421nipeni kero zenu nitazishughulikia,"ameongeza.

Amesema kwa Watendaji wa Serikali ambao wanafanya kazi chini yake wajipange kisawasawa kufanya kazi kuwahudumia Wananchi, na kwamba wakizembea Matatizo yao atayapata kupitia namba yake ya Simu na atafika eneo husika kuitatua.
Nao baadhi ya Wananchi wa Oldshinyanga wametoa kero zao kwa Mkuu wa Wilaya,zikiwamo za Migogoro ya Mipaka, Urasimishaji maeneo,ukosefu Mashamba ya Kilimo,ulipwaji Fidia Mradi SGR, na Malipo Sh.milioni 2.6 kwa wananchi waliokuwa wakisomba Mchanga ujenzi Sekondari Oldshinyanga tangu mwaka 2018,na eneo la Tanganyika Packers.

Kero zingine kuchelewa ulipwaji fidia kupisha ujenzi wa Barabara Kiwango cha Lami kutoka Oldshinyanga hadi Solwa, na hivyo kushindwa kufanya Shughuli zingine ikiwamo ujenzi wa nyumba, sababu tathimini imeshafanyika zaidi ya miaka miwili sasa,kero za Maji na Wajawazito kutozwa fedha kwa ajili ya kujifungua,na uuzaji Mazao kwa Mfumo wa Stakabadhi gharani na kucheleweshewa malipo.
Kero zote ambazo zimewasilishwa na wanannchi zimepatiwa majibu na Wakuu wa Idara husika pamoja na Mkuu wa wilaya na kutatuliwa,pamoja na zingine kuahidiwa kufuatiliwa.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza na Wananchi wa Kata ya Old Shinyanga katika kusikiliza kero zao na kuzitatua.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza na Wananchi wa Kata ya Old Shinyanga katika kusikiliza kero zao na kuzitatua.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe akizungumza kwenye Mkutano wa kusikiliza kero za Wananchi wa Oldshinyanga.
Diwani wa Vitimaalum Tarafa ya Oldshinyanga Pica Chogelo akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akichukua kero za wananchi
Wananchi wa Oldshinyanga wakiwasilisha kero zao kwa Mkuu wa Wilaya.
Wananchi wa Oldshinyanga wakiendelea kuwasilisha kero zao.
Wananchi wa Oldshinyanga wakiendelea kuwasilisha kero zao.
Wananchi wa Oldshinyanga wakiendelea kuwasilisha kero zao.
Wananchi wa Oldshinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro wa kusikiliza kero zao na kutatuliwa.
Mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za Wananchi wa Kata ya Oldshinyanga ukiendelea.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464