WEADO WAMEFANYA MAJADILIANO JUU YA MILA NA DESTURI CHANYA ZENYE KUZINGATIA USAWA WA KIJINSI KWA KUZUIA UKATILI,KATA YA LYABUKANDE WILAYANI SHINYANGA
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
SHIRIKA la Women Elderly Advocacy and Development Organization (WEADO)ambalo linatetea haki za Wanawake na Watoto mkoani Shinyanga, limefanya Majadiliano na Makundi mbalimbali ya viongozi na kijamii Kata ya Lyabukande wilayani Shinyanga,juu Mila na Desturi chanya zinazochochea usawa wa Kijinsi.
Shirika hilo la WEADO lipo kwenye utekelezaji wa Mradi wa chukua hatua sasa,zuia ukatili kwa Awamu ya Pili chini ya ufadhili wa Shirika la Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust) ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miezi Sita unaoanzia Machi hadi Agosti Mwaka huu.
Majadiliano hayo yamefanyika leo April 5,2024 katika Shule ya Msingi Lyabukande na kushirikisha viongozi wa kidini, Mila, vyama vya siasa,Wazee Maarufu,Jukwaa la Wanawake, Vijana,Watu wenye ulemavu,Watendaji wa Kijiji, Kata na Diwani wa Lyabukande Luhende Kawiza.
Mratibu wa Mradi huo John Eddy kutoka Shirika la WEADO, amesema utekelezaji wake ni Awamu ya pili hivyo kwa sasa wamejikita zaidi kwenye uchukuaji wa hatua ili kutokomeza ukatili kabisa wa Kijinsi na jamii Ibaki kuwa salama.
Amesema katika utekelezaji wa Mradi huo kwa Awamu hii,watajikita zaidi katika Masuala ya Mila na Desturi chanya ndani ya jamii, zisizo chochea ukatili dhidi ya Wanawake,watoto,bali ziwe na mlengo wa kuzingatia usawa na mahitaji ya kijinsi.
"Mradi wetu huu wa chukua hatua sasa,zuia ukatili kwa Awamu hii ya pili, tutajikita pia katika Masuala ya Mila na Desturi zinazo zingatia usawa wa Kijinsi, jamii jumuishi na ujenzi wa mazingira salama yasiyo na viashiria vya ukatili wa Kijinsi," amesema John.
Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko,amesema wanatekeleza Mradi kwa Awamu ya pili katika Kata hiyo ya Lyabukande ili kutokomeza kabisa ukatili wa Kijinsi na kuleta usawa ndani ya jamii.
Amesema watapita pia katika maeneo ya Afya,Mazingira, Lishe Bora na Kilimo, na kwamba Malengo ya Mradi huo ni kupata hali ya usawa wa Kijinsi kwa kutokomeza kabisa ukatili ndani ya jamii dhidi ya Wanawake na Watoto.
Nao Washiriki wakichangia Majadiliano, wamesema siyo zote Mila na Desturi ni Mbaya, bali zipo ambazo ni nzuri zikiwamo za kulinda Maadili ndani ya jamii,huku wasisitiza zile ambazo ni mbaya jamii inapaswa kuelimishwa na kuziacha.
Aidha,katika kikao hicho Washiriki walipitisha Maazimio juu ya kuzuia vitendo vya ukatili vitokanavyo na kuendekeza Mila na Desturi Kandamizi, kwamba Mzazi akibainika kuozesha Mtoto achukukuliwe hatua za kisheria pamoja na kutengwa na jamii,pamoja na watoto wote waandikishwe na kuhitimu.
Azimio jingine la ukatili wa Kimwili kwa vipigo kwa Wanawake, watozwe faini za Kijiji na kupelekwa Mahakamani, pia suala la Ugawanyaji mali kwa wana ndoa wanaofarakana sheria zizingatiwe na kutolewa haki kwa usawa bila upendeleo wa kijinsi.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko akizungumza kwenye Mjadala huo kwa kuelezea utekelezaji wa Mradi.
Mkurugenzi wa Shirika la WEADO akiendelea kuzungumza kwenye Mjadala huo.
Mkurugenzi wa Shirika la WEADO akiendelea kuzungumza kwenye Mjadala huo.
Mratibu wa Mradi wa chukua hatua sasa,zuia ukatili kutoka Shirika la WEADO John Eddy akielezea namna ya utekelezaji wa mradi huo.
Mratibu wa Mradi wa chukua hatua sasa,zuia ukatili kutoka Shirika la WEADO John Eddy akielezea namna ya utekelezaji wa mradi huo.
Afisa ufuatiliaji na Tathimini wa mradi huo kutoka Shirika la WEADO Kadeth Geogre akizungumza kwenye mjadala huo.
Diwani wa Kata ya Lyabukande Luhende Kawiza akizungumza kwenye mjadala huo.
Washiriki wakiwa kwenye Mjadala huo.
Washiriki wakiendelea na mjadala kupitia kazi ya vikundi.
Washiriki wakiwa kwenye Mjadala huo.
Washiriki wakiwa kwenye Mjadala huo.
Washiriki wakiendelea na mjadala kupitia kazi ya vikundi.
Washiriki wakiendelea na mjadala kupitia kazi ya vikundi.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464