Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara kwa mara nyingine imetupilia mbali shauri la rufaa ya jinai namba 577 la mwaka 2024 lilikuwa linamuhusu Hashimu Ally ambaye ni mrufani dhidi ya Pauline Gekul ambaye alikuwa ni mrufaniwa.
Pauline Gekul
Mahakama hiyo ilitiishwa kwa ajili ya kutoa uamuzi wa mapingamizi na sababu za rufaa ambazo awali ziliwasilishwa na kusikiliza Mahakamani.
Hayo yamebainishwa April, 15.2024, mbele ya Mheshimiwa Jaji Devotha Kamuzora, aliyesikiliza rufaa hiyo namba 577/2024.
Katika rufaa hiyo Ally anapinga uamuzi uliofanywa na Mahakama ya Wilaya ya Babati Desemba 27,2023 ya kuiondoa kesi hiyo mahakamani baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.
kabla ya kusikilizwa rufaa hiyo, Mahakama hiyo ilisikiliza pingamizi za awali zilizowasilishwa na upande wa mjibu maombi, kisha kusikiliza hoja sita zilizowasilishwa na upande wa mleta rufaa ambapo Mahakama hiyo imeridhika kati ya sababu tatu na mapingamizi yaliyoletwa Mahakamani na mjibu rufani Pauline Gekul sababu moja imetosha kuondoa shauri hilo.
Awali, Paulina ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria kabla ya kutenguliwa Novemba 25,2023, alidaiwa kumshambulia na kumdhuru Hashim Ally novemba 11,2023 kinyume cha kifungu cha 41 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya 2022.
Mrufani Hashimu Ally kupitia mawakili wake Peter Mageleka, Tadei Lista na Joseph Masanja walibainisha kuwa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara ililiita shauri la jinai namba 577 la mwaka 2024 mbele ya Mheshimiwa jaji Devota Kamuzora na kwamba wanatarajia kukataa rufaa Mahakama ya rufani Tanzania.
Shauri hilo lilisikilizwa lakini kama ilivyo taratibu wa kisheria tarehe 20 Machi 2024 mrufaniwa Pauline Gekul alisajili pingamizi la awali Kwa maana ya kutoa notisi la pingamizi la awali Mahakamani kwa kuweka mapingamizi matatu akipinga rufaa hiyo kusikiliza.
Mawakili hao katika kupinga mapingamizi hayo matatu walibainisha kuwa hayana mashiko kwakuwa Mahakama hiyo Ina mamlaka ya kisheria kupokea rufaa zote zinazotokana na maamuzi za Mahakama za chini.
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO EATV
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464