KISHAPU WAPANDA MITI,WAFANYA USAFI WA MAZINGIRA KUADHIMISHA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

KISHAPU WAPANDA MITI,WAFANYA USAFI WA MAZINGIRA KUADHIMISHA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

Na Marco Maduhu,KISHAPU
MKUU wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude,ameongoza Wananchi wa Wilaya hiyo kupanda Miti pamoja na kufanya Usafi wa Mazingira katika maeneo ya huduma za Afya, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Zoezi hilo la kupanda Miti pamoja na kufanya Usafi wa Mazingira, limefanyika leo Aprili 20,2024, katika Kituo cha Afya Kishapu pamoja na Hospitali ya wilaya hiyo ya Kishapu "Jakaya".
Mkude amesema,Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Sherehe kubwa,ambayo inaunganisha pande zote mbili kuwa wamoja pamoja na kudumisha Amani,kwa kuwaenzi waasisi wake Abeid Amani Karume na Mwalimu Julius Nyerere, ambapo Kishapu wameamua kuuenzi Muungano kwa kupanda Miti, na kufanya usafi wa Mazingira.

Amesema Mbali na upandaji huo wa Miti na kufanya Usafi wa Mazingira, pia watafanya Makongamano mbalimbali na Mabonanza ya Michezo, ambayo atakuwa na mijadala na utoaji wa Elimu juu ya faida ya kuwa na Muungano, na kwamba Siku ya Aprili 25 kutakuwa na Mkesha Mkubwa wilayani humo kusherehekea Muungano.
"Wilaya ya Kishapu tumeamua kuadhimisha sherehe za Muungano kwa kufanya Shughuli za Kijamii, kwa kupanda Miti,kufanya Usafi wa Mazingira, kutoa Elimu ya Faida ya Muungano kupitia Makongamano na Mabonanza ya Michezo," amesema Mkude.

"Katika zoezi la upandaji Miti kwa leo tumepanda Miti zaidi ya 2,000 ikiwamo ya Matunda na Kivuli, na tunaushukuru pia Mgodi wa Williamson Diamonds WDL, kwa kutuunga Mkono katika suala la utunzaji Mazingira na kutupatia Miti ya kupanda,"ameongeza Mkude.
Aidha, amewataka pia Wananchi wa Kishapu kuendelea kutunza Mazingira pamoja na vyanzo vya Maji, na kuacha kukata Miti hovyo kwa ajili ya kuni, bali wabadilike na kutumia Nishati Safi ya kupikia.

Afisa Mazingira wilayani Kishapu Jamila Nambimbi,amesema hali ya upandaji Miti wilaya ya Kishapu ni nzuri,ambapo kwa Mwaka huu tayari wameshapanda Miti zaidi ya Laki Moja ikiwamo ya Matunda, na kutoa wito kwa wananchi wilayani humo waendelee kupanda Miti kwa wingi ili kutunza Mazingira pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha,Kilele cha Sherehe cha Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni April 26, 2024, Sherehe ambazo hufanyika kila mwaka Aprili 26.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akiongoza zoezi la upandaji Miti katika kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambacho kilele chake ni Aprili 26,2024
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akiongoza zoezi la upandaji Miti katika kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akiongoza zoezi la upandaji Miti katika kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Picha ya pamoja ikipigwa katika zoezi hilo la upandaji Miti.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464