KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO SHINYANGA LIMETOA MAFUNDISHO YA AFYA,BIASHARA,KAYA NA FAMILIA KATIKA SEMINA MAALUMU
KANISA la Waadventista Wasabato Shinyanga limeendesha Semina Maalumu,ambayo imekutanisha watu mbalimbali na kutoa Mafundisho ya Afya,Biashara pamoja na Kaya na Familia.
Semina hiyo ya Jimbo (NGBF) imeanza kutolewa leo Aprili 21,2024 ambayo katika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya Makindo iliyopo katikati ya Mji wa Shinyanga, ambayo itaendeshwa kwa muda wa wiki nzima hadi Aprili 27 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Semina hiyo Dk. Herison Maeja, amesema lengo lake ni kukatanisha watu mbalimbali, kufahamiana pamoja na kupata Mafundisho kutoka kwa Wataalamu wa Afya, Wabobezi wa Biashara pamoja na Masomo ya Kaya na Familia.
Amesema kwa upande wa Wataalamu wa Afya watakuwepo Madaktari Bingwa akiwamo Dk.Luzila, Igenge, Asnathi,Maufi na Madanka, ambapo Somo la Biashara litakuwa likitolewa na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Shinyanga (TCCIA) Jonathani Manyama, huku Somo la Kaya na Familia litatolewa na Mchungaji Mstaafu Wilbert Nfumbusa.
“Tunawakaribisha wakazi wa Mkoa wa Shinyanga wahudhurie kwenye Semina hii ambayo ni muhimu sana katika maisha yao ya kila siku ili wapate kujifunza masomo mbalimbali na kubadili mwenendo wa maisha yao,”amesema Dk.Maeja.
Aidha,Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaaa Mkoa wa Shinyanga Dk.Luliza John, akitoa Somo la Magonjwa yasiyo ya kuambukiza,amewataka wananchi kujenga tabia ya kupima Afya zao Mara kwa Mara sababu Magonjwa hayo hayana dalili.
Amesema Mgonjwa yasiyo ya kuambukiza huchagia Vifo vya watu wengi, ambayo mara nyingi hushambulia Moyo, huku akitaja visababishi vyake kuwa ni Matumizi ya Tumbaku, Ulevi uliokithiri,kutofanya mazoezi,kutozingatia Mlo kamili, na uchafuzi wa hali ya hewa.
Naye Mchungaji Mstaafu Wilbert Nfumbusa, akitoa Somo la Kaya na Familia, ametaja Siri kubwa 4 za kufanya Familia kuwa na Furaha, ambapo ni kujipenda wewe mwenyewe, kumpenda Mwenzi wako kama nafsi yako, kumpenda Mwanao kama sehemu ya yako mwenyewe,pamoja na kumpenda Mungu kuliko vitu vyote.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mwenyekiti wa Semina Dk.Herson Maeja akizungumza kwenye Semina hiyo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dk.Luzila John akitoa Soma la Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwenye Semina hiyo.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Shinyanga (TCCIA)Jonathan Manyama akitoa Somo la Biashara kwenye Semina hiyo.
Mchungaji Mstaafu Wilbert Nfumbusa, akitoa somo la Kaya na Familia kwenye Semina hiyo.
Mchungaji wa Mtaa Kanisa la Wasabato Shinyanga Mjini Gadiel Mziray akifuatilia Semina hiyo.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Kwaya ya Walawi ya Kanisa la Wasabato Shinyanga Mjini ikiimba kwenye Semina hiyo.
Kwaya ya Walawi ya Kanisa la Wasabato Shinyanga Mjini ikiimba kwenye Semina hiyo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464