Wanafunzi 80,000 wakosa masomo kisa mafuriko
Zaidi ya wanafunzi 80,000 wa shule za msingi katika wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani wamekosa masomo kufuatia mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Ofisa Elimu mkoa wa Pwani, Sara Mlaki, ameyasema hayo kwenye ziara ya kujionea athari za mvua hizo katika shule na makazi katika wilaya za Rufiji na Kibiti ikiwamo kuharibu miuondombinu ya elimu.
Amesema shule 11 za msingi zenye wanafunzi 7,264 wakiwemo wasichana 3,657 na wavulana 3607 wameathirika na mafuriko wilayani Rufiji.
Aidha nyumba 58 za walimu pia zimeathiriwa na kupoteza samani na mali zilizokuwemo ndani ya nyumba hizo.
Amesema katika wilaya ya Kibiti wanafunzi 824 katika shule 7 za msingi zimeathirika huku 3 zikifungwa kutokana na adha hiyo huku sekondari ya Mtanga Delta ikiathirika pia.
Akizungumzia maafa hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolph Mkenda, alisema tayari serikali imeweka utaratibu kwa wanafunzi wote waliokumbwa na mafuriko hayo kusoma kwenye shule maalum ambazo zimetengwa.
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO EATV
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464