YOUNG WOMEN LEADERSHIP,WASHIRIKIANA NA SERIKALI WILAYANI SHINYANGA KUHUISHA MABARAZA YA WATOTO SHULENI
SHIRIKA la Young Women Leadership (YWL) kwa kushirikiana na Serikali wilayani Shinyanga,wameanza kuhuisha Mabaraza ya watoto Shuleni,ili kusaidia upatikanaji wa taarifa za ukatili na kuwachukulia hatua wahusika na kukomesha vitendo hivyo.
Zoezi hilo la kuhuisha Mabaraza ya watoto shuleni,linakwenda Sambamba na uhuishaji Madawati la ulinzi na usalama kwa watoto walio ndani ya shule na nje ya shule, ambapo leo Aprili 29 limefanyika katika Shule ya Msingi Ng'homango.
Mratibu wa Shirika la Young Women Leadership Veronica Masawe,akizungumza kwenye zoezi hilo, amesema Mabaraza hayo ya watoto pamoja na Madawati la ulinzi na usalama, wanayahuisha katika Kata mbili ya Nyamalogo na Iselamagazi kwa ufadhili wa Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust).
Naye Mratibu wa Mpango Mkakati wa Serikali wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA)wilayani Shinyanga Aisha Omary, amesema Mabaraza hayo ni chachu kubwa katika kupunguza vitendo vya ukatili kwa watoto, sababu watakuwa huru kutoa taarifa za ukatili kupitia viongozi wao au Sanduku la Maoni.
“Uhuishaji wa Mabaraza ya Watoto na Madawati ya ulinzi na usalama kwa Mtoto,utasaidia kupata taarifa kwa urahisi za ukatili dhidi ya watoto, sababu watakuwa wakipeana taarifa kupitia viongozi wao ambao ni watoto wenzao, na hawawezi kuogoga kama ilivyo kutoa taarifa kwa watu wazima, na itasaidia kupunguza ukatili,”amesema Aisha.
Amewataka pia wanafunzi wasitunze siri juu ya vitendo vya ukatili ambayo hufanyiwa, bali watoe taarifa kwa viongozi wao wa Mabaraza ,au kwa Walimu,Watendaji,Maofisa Maendeleo na hata wazazi, na endapo wakishindwa kabisa, watoe taarifa kwa kuandika Memo na kuweka kwenye Sanduku la Maoni.
Nao baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Ng'homango Kata ya Iselamagazi Sophia Silas, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Watoto shuleni hapo, amesema baraza hayo yana msaada mkubwa kwa watoto kutoa taarifa za ukatili, sababu ni watoto wenzao na wanakuwa hawana uoga wa kutoa taarifa.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mratibu wa Mpango Mkakati wa Serikali wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA)wilayani Shinyanga Aisha Omary akitoa elimu ya Mabaraza ya watoto katika Shule ya Msingi Ng'homango Kata ya Iselamagazi wilayani humo.
Mratibu wa Shirika la Young Women Leadership Veronica Masawe akizungumza kwenye zoezi hilo la uhuishaji Mabaraza ya watoto shuleni.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ng'homango Kata ya Iselamagazi wilayani Shinyanga wakiwa kwenye Uhuishaji wa Mabaraza ya Watoto na Madawati ya ulinzi na usalama kwa mtoto shuleni hapo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ng'homango Kata ya Iselamagazi wilayani Shinyanga wakiwa kwenye Uhuishaji wa Mabaraza ya Watoto na Madawati ya ulinzi na usalama kwa mtoto shuleni hapo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ng'homango Kata ya Iselamagazi wilayani Shinyanga wakiwa kwenye Uhuishaji wa Mabaraza ya Watoto na Madawati ya ulinzi na usalama kwa mtoto shuleni hapo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ng'homango Kata ya Iselamagazi wilayani Shinyanga wakiwa kwenye Uhuishaji wa Mabaraza ya Watoto na Madawati ya ulinzi na usalama kwa mtoto shuleni hapo.
Zoezi la Uhuishaji Baraza la Watoto na Dawati la Ulinzi na Usalama wa Mtoto likiendelea katika Shule ya Msingi Ng'homango wilayani Shinyanga.
Viongozi wa Baraza la Watoto na Dawati la Ulinzi na usalama wa Mtoto ambao wamechaguliwa katika Shule ya Msingi Ng'homango wilayani Shinyanga.
Mratibu wa MTAKUWWA Wilayani Shinyanga Aisha Omary, akiwa na Mratibu wa Shirika la YWL Veronica Masawe wakitoa elimu kwa vitendo kwa wanafunzi juu ya kupinga ukatili na wasikubali kushikwa kwenye viungo vyao (Don't Touch apa kwangu).
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464